Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Maneja msaidizi wa huduma za kifedha Bank Kuu Angela Abayo amesema kama Benki Kuu wanashiriki maonesho ya nane nane kanda ya kati kutoa elimu kwa wananchi kutambu huduma na shughuli zinazofanywa na Bank hiyo.


Bi.Abayo amesema hayo Leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alipotembelea Banda la Benki Kuu katika sherehe za maonesho ya Nanenane kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni Dodoma.


Amesema Benki kuu linajukumu kubwa la kuhakikisha bei za mazao yanayotumika kwa wingi hazibadiliki sana na kudhibiti mfumuko wa bei.


Amesema Benki Kuu linasimamia suala la Mfumuko wa bei kwasababu mfumuko wa bei unaathiri maisha ya watu moja kwa moja wakiwemo wakulima na Wafugaji.


Aidha amesema Benki Kuu inaandaa na kutekeleza Sera ya fedha kwania ya kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuangalia kiwango cha fedha kilichopo kwenye mzunguko lazima kiendane na mahitaji ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.


Katika hatua nyingine Bi. Abayo amesema ujazi wa fedha ukizidi mahitaji ya kuendeshea shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo Kilimo na ufugaji bei za vitu zinaweza kuongezeka na kuathiri hata wawekezaji nchini.


“Muwekezaji akikatishwa tamaa akafunga pale serikali itakosa pato la taifa itakosa Mapato ambayo inakusanya kwamaana ya Kodi na hata kiwango cha uzalishaji hushuka pia na huyu ni muwekezaji unaweza kuwa ameajiri kwahiyo hata hizo ajira zinaweza zikapotea. ” Amefafanua Bi. Abayo


Ameeleza kuwa ni muhimu Benki Kuu kudhibiti mfumuko wa bei kwa kudhibiti kiasi cha ujazo wa fedha.



Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: