Na Immnauel Msumba, Arusha


Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi. amesisitiza wakandarasi watatu na mshauri mmoja waliosaini mradi wa sh, bilioni 7.282 kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wapate maji ikiwemo kuwatua ndoo kichwani wanawake na wananchi kwa ujumla.

Mhandisi Mahundi ametoa rai hiyo Jana Jijini Arusha katika halfa ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini.

Alisema  miradi hiyo ni lazima ikamilike kwa wakati na serikali inauwezo wa kutumia wazawa katika kufanikisha hatua mbalimbali za miradi ya maji hususan ya vipuri.

Aliwasihi wakandarasi wazawa kuonyesha juhudi zao katika miradi mbalimbali wanayopewa ili kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwemo ufikishaji wa maji katika maeneo mbalimbali ili shughuli za kiuchumi zifanikiwe na kufika kila mahali.

"Tunampongeza Rais Samia kwa miradi mikubwa anayofanya ikiwemo suala la bandari lakini tutahakikisha hatumkwamishi tunasambaza maji ili kupeleka maendeleo kwa wananchi"

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema serikali ya awamu ya sita inafanya mambo mbalimbali ya kuleta maendeleo Mkoani Arusha na kusisitiza kuwa serikali inasimamia zaidi maslahi mapana ya watanzania.

"Rais Samia anazidi kuketa miradi inayoondoa changamoto za watu wa Arusha na kwa miradi hii ni taswira tosha ya huduma zilizolengwa"

 Ambapo Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),Mhandisi Joseph Makaidi alisema miradi mitatu ni ya ujenzi wa miundombinu na mradi mmoja ni wa mtaalam mshauri Bene Consult (T) Ltd 

Miradi hiyo  minne yenye thamani ya sh,bilioni 7.282  inatekelezwa maeneo manne ambayo ni mradi wa maji ambapo utekelezaji wa mikataba hiyo itakayohudumia watu zaidi ya 54,000 watanufaika .

Huku Mkandarasi mshauri wa kampuni ya Bene Consult (T)LTD ,Bernard Msaday aliishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kuifanya kadri ya utaalam wao ulivyo katika kuhakikisha wananchi wanapata maji huku mwakilishi wa kampuni ya Jandu,Nitu Jandu alisema nafasi walizopewa watazifanyia kazi ili kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati

Huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha , Zelothe Steven  alisema Mkoa wa Arusha unajivunia fursa mnalijua za miradi ikiwemo mradi huo wa maji unaotatua changamoto za wananchi katika sekta ya maji.

Miradi hiyo minne wa kata ya Uwiro na kijiji cha Engatukoit wenye thamani ya sh,bilioni 1.877  wilayani Arumeru unatekelezwa na mkandarasi  M/s Gopa Contractors Tanzania Limited wa pili ni ukarabati wa mradi wa maji vijiji vya Endonyawet na Matala  wilayani Karatu wenye thamani ya sh,milioni 839.618 unaotekelezwa na mkandarasi M/s Climax Unit Limited

Mradi mwingine ni uboreshaji wa maji Pori Tengefu la Poloreti wilayani Ngororongoro katika vijiji vya Ngobereti,Oloipir,Soitsambu,Losoito,Arash,Loswash,Kirtali,Mondoros,Sukenya,Orokanda na Olaika wenye thamani ya sh, bilioni 3.553 ,ambapo kampuni ya M/s Jandu Plumbers Limited itatekeleza

Na mradi wa nne ni wa ushauri wa kitaalam kwaajili ya usanifu wa miradi ya maji kwa wilaya  ya Arumeru,Monduli ,Karatu na Longido wenye thamani ya sh bilioni 1.011 kutoka kampuni ya M/s Bene Consult (T) Ltd.




Share To:

Post A Comment: