DENIS CHAMBI, MARA.
KILIMO
kinalipa! ndicho unachoweza kusema unapotaka kumzungumzia Nyihita
Wilfred mwekezaji mzawa aliyejikita kwenye sekta ya kilimo kupitia zao
la Alizeti katika Kijiji Nyanchabakenye Wilaya ya Rorya mkoani Mara
ambapo sasa amekuwa mwarobaini kwa wakulima wengine ambao wamepata soko
la kuweza kuuza mazao yao baada ya kuanzisha kiwanda cha kuchakata zao
hilo la mafuta Nyihita Sunflower Cooking oil Production.
Mbali
na mapinduzi ya kiwanda hicho alichokijenga kwaajili ya kuchakata zao
hilo na kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta yayokanayo na Alizeti lakini
pia ameweza kufungua na kutoa ajira kwa vijana hatua ambayo ni ya
kujivunia kwa wana Mara ambao hujipatia kipato chao kutokana na
uwekezaji huo.
Mwekezaji
huyo anasema aliigeuza changamoto na kuwa fursa kwake hii ni kutokana na
kukosekana kwa kiwanda cha zao la Alizeti ndani ya mkoa huo na hivyo
kupata wazo la kuja na sasa ana miliki kiwanda cha kuzalisha mafuta ya
kula yatokanayo na zao hilo alichokipa jina lake la Nyihita Sunflower
Cooking oil Production.
"Nilipata
wazo la kuja kufanya uwekezaji wa kilimo cha Alizeti ndani ya mkoa wa
Mara ikiwa ni eneo ambalo halikiwahi kuwa na historia ya kilimo cha
Alizeti na niliamini kwamba malighafi zinapatikana kijijini na maendeleo
makubwa na mapinduzi ya viwanda yanafanyika vijijini."
"Nialiamua
kuja vijijini ambako niliamini ninaweza kuja kuwashawishi wakulima
ambao mashamba yapo ili waweze kulima na ni kweli wazo hili lilifanikiwa
kwa asilimia 100 kwani wakulima walijitokeza na kuanza kulima kilimo
cha Alizeti mwaka 2019, na ilipofika 2020 wakulima walianza kujiuliza
maswali mara baada ya kulima mazao tutauza wapi nikapata wazo kwa
kutafuta wazo la soko na kujenga kiwanda baada ya kuanza ujenzi huo
kiwanda hiki kilizinfuliwa rasmi 2021 na kiongozi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru kitaifa na ndio kikaanza kufanya kazi mpaka sasa" alisema
Anasema
anajivunia kuwa mwekezaji mzawa na mmoja wa watanzania ambao wanaweza
kuzalisha fursa za ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo sambamba na
kuwapatia soko la uhakika wakulima hatua ambayo imekuja kuleta mwamko
wa wakulima wengi kujikita shambani tofauti na ilivyokuwa awali.
"Pamoja
na hayo uwepo wa kiwanda hiki kimeweza kutengeneza fursa za ajira kwa
vijana wetu wa kitanzania lakini pia kuongeza uchumi wa mtu mmoja
mmoja kwahiyo tumeongeza wigo mpana kwa ndugu zetu wa Mara kuweza
kuongeza pato lao kupitia kiwanda hiki na wakulima kuweza kupata soko la
uhakika na kuuza malighafi zao hapa na pia kiwanda hiki kimeweza kuwa
faida kwa nchi yetu ya Tanzania kwani tunalipa kodi na zinasaidia
kuleta maendeleo kwenye Taifa letu" aliongeza mwekezaji huyo.
"Ni
wito wangu kwa watanzania na wana Mara kujikita kwenye kilimo cha
Alizeti wakitumie kama fursa na kuhakikisha tunasaidia kuinua uchumi wa
Taifa letu lakini pia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja ndani ya
Tanzania kwa ujumla" alisisitiza.
Nyihita
anasema ukubwa wa kiwanda hicho hauendani sawa na mali ghafi
inayozalishwa mashambani ambayo imekuwa ni mdogo hatua ambayo amewaasa
wananchi kuendelea kujikita katika kilimo hicho kwani tayari uhakika wa
wapi watauza mazao yao upo ni suala tu la kuongeza uzalishaji.
"Uwezo
wa kiwanda ni mkubwa tofauti na Malighafi inayoweza kupatikana, kwa
misingi hiyo basi tunahitaji wakulima wajitokeze kwa wingi kulima
wakijua kwamba fursa ya soko la uhakika ipo ili waweze kusaidia kiwanda
kuweza kuzalisha kwa wingi na kupata ukamilifu wa uhitaji wa mali ghafi"
"Sasa
hivi wizara ya kilimo imeanzisha kilimo biashara wazo hili linasaidia
vijana wakitanzania na watanzania kwa ujumla kuweza kujikita kwenye
kilimo kwahiyo kupitia wazo hili la kilimo biashara litasaidia
watanzania kujiwekeza ni matumaini yangu kwamba kupitia kilimo biashara
vijana wengi watajitokeza kulima zao hili ambalo litasaidia kuongeza
utoshelevu wa uhitaji wa malighafi"
Meneja
wa kiwanda hicho cha Nyihika Sunflower Cooking oil Production
Happiness Masunga alisema wakiwa na uwezo wa kuajiri watu mbalimbali
kwa siku kina uwezo wa kuchakata tani 24 lakini kutokana na changamoto
ya upatikanaji wa malighafi kwa sasa wanazalisha chini ya kiwango
hado asilimia tano kwa siku.
"Mchakato
wa Kiwanda hiki ulianzia mwaka 2019 kama sehemu ya uhamasishaji wa
kilimo uwezo soko Ia Alizeti kwa wakulima wa Mara na ilipelekea
kuanzishwa kwa kiwanda hiki 2021 na sasa kinatambulika na serikali na
kuajiri watu mbalimbali, kiwanda hiki kwa siku kina uwezo kuchata hadi
tani 24 lakini kutokana na ukosefu wa malighafi za kutosha sasa hivi
uchakataji wake umeshuka sana hadi asilimia tano" alibainisha meneja
huyo.
Mariam Hamis ni
miongoni mwa waajiriwa wa kiwanda hicho anasema
"Vijana wengi tunafaidika na kunufaika na uwepo wa kiwanda hiki
kutupatia ajira ambapo watu waliosoma na wasio soma wameweza kuajiriwa
katika kiwanda cha Nyihita Sunflower Cooking oil Production na kimeweza
kupunguza upungufu wa ajira ambalo ni tatizo bado katika nchi yetu,
uwepo wa kiwanda hiki umekuwa na manufaa kwa wananchi wengi".
Mkurugenzi wa kiwanda cha Nyahita Sunflower Coking Oil Production Nyihita
Wilfred akimkabidhi mafuta ya Alizeti mwandishi wa habari Ibrahim Kunoga wakati alipomtembelea katika kiwanda chake kujifunza namna jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi.
Meneja wa kiwanda hicho cha Nyihika Sunflower Cooking oil Production Happiness Masunga akiwaongoza wageni waliotembelea kiwandani hapo kujua na kujifunza namna jinsi kinavyofanya kazi ya uzalishaji wa mafuta ya kupikia yatokanayo na zao la Alizeti.
Post A Comment: