Na  Magesa Magesa,Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha,CPA Amos Makalla amewataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29 huku akiwahakikishia wananchi kuwa hakuna hali yeyote ya uvunjifu wa amani utakaojitokeza kwani Mkoa umejipanga vizuri.

Ameyasema hayo leo mjini hapa alipokuwa akizungumza na wazee wa mkoa wa Arusha mara baada ya kupokea matembezi ya kilometa mbili ya wazee hao yaliyolenga kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

CPA Makalla amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Arusha kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na siku ya kupiga kura na kusema kuwa yeye kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa mkoa uko salama kabla,wakati na hata baada ya uchaguzi.

Nawahakikishia wazee wangu kama mlivosema katika risala yenu  mnaomba amani na utulivu katika Mkoa huu,na mimi niwaambie kuwa pamaja na kazi nyingine alizonazo Mkuu wa Mkoa,ila kazi ya kwanza ni kuhakikisha kuwa Mkoa unakuwa salama wati wote,hivyo niwatoe hofu wazee wangu”alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa

Awali katika risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Mwenezi wa Taifa wa Chama Cha Wazee Wanaume Tanzania(CCWWT) Sabas Kisakeni waliiomba Serikali kuwapatia bima ya afya bure wazee waote haa nchini pamoja na kuhakikisha kuwa inawalinda kutokana na umri walionao.

“Wazee hapa nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi sana ila kubwa zaidi ni kuzorota kwa afya yao kutokana na kunyemelewa na maradhi mbalimbali kutokana na umri wao hivyo tunaiomba Serikali kuwatatulia wazee changamoto hii kwa kuwapatia matibabu bure au kuwapatia bima za afya”alisisitiza Kisakeni.

Aliongeza kuwa  matembezi hayo ya kilometa mbili yaliwashirikisha wazee zaidi ya mia tano na kwamba ilikuwa ni sehemu ya mazoezi kwa wazee hao na kuwa  wazee walipita katika maeneo mbalimbali ya kihistoria jijini Arusha.

Matembezi hayo ya wazee kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Arusha,yaliandaliwa na Chama cha Wazee Wanaume TanzaniaCCWWT),Chama cha Wazee Mkoa wa Arusha(CHAWAMA)na Umoja wa wazee Mkoa wa Arusha kwa kuratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo wazee walipata fursa ya kuchunguzwa magonjwa ya macho bure.

Share To:

Post A Comment: