Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Martha Mlata, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mwamagembe katika mkutano wa hadhara alioufanya baada ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Julai 29, 2023.

Na Dotto Mwaibale, Manyoni

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Martha Mlata ameiagiza Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni kupeleka madawati katika Shule Mpya ya Sekondari ya Mwamagembe kabla ya Agosti 15, 2023 ili wanafunzi waanze masomo.

Mlata ametoa agizo hilo leo Julai 29, 2023 wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara ambapo alipokea kero mbalimbali za wananchi wa Kata hiyo..

"Niseisikia taarifa yenu kuwa wanafunzi wa kata hii wanalazimika kutembelea kilomita 70 kwenda Rungwa kwa ajili ya kusoma jambo hili haliwezekani kwani linawatesa watoto nakuagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi hakikisheni kabla ya Agosti 15, 2023 muwe mmeleta madawati hapa shuleni wanafunzi waanze masomo," alisema Mlata.

Aidha Mlata alimwagiza Afisa Tarafa wa Itigi, Eliutha Augustone kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota ili awasiliane na viongozi wa idara ya elimu wafanye uteuzi wa Mkuu wa Shule hiyo kuhakikisha anamteua Mkuu wa Shule hiyo.

Mlata alisema alichobaini ukanda huu wa Kata za Mawamagembe zimesauliwa sana kielimu na kuagiza nguvu zaidi ziwekezwe ili kuhakikisha watoto wanapata elimu kama ilivyo kata zingine.

Diwani wa Kata hiyo, Jonathan Dulle akielezea changamoto ya shule hiyo kutoanza kutumumika kutokana na sababu mbalimbali na kwamba mwaka jana wanafunzi waliofaulu na kuanza masomo katika Shule ya Sekondari ya Rungwa walikuwa 96 wanaoendelea na masomo ni sita na waliohama ni 46 na kuwa wanafunzi 44 hawajulikani walipo.

Mlata baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo alifanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniface, akizungumza kwenye mkutano hau ambapo alisikitishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itigi kushindwa kuhudhuria ziara yake.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Yohana Msita, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Elphas Lwanji akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Martha Mlata, akipokelewa na viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
















 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: