Na John Walter-Babati
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani wa Manyara Yustina Rahhi ametoa misaada mbalimbali kwa ajili ya wafungwa wa Gereza la Babati.

Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo jumanne 25/07/2023 katika Gereza hilo lililopo Mrara  mjini  Babati  yakishirikisha viongozi wa  Jumuiya ya Wanawake (UWT) mkoa na Wilaya.

Misada iliyotolewa na Mbunge ni pamoja na Sukari, Mafuta ya kujipaka,Sabuni,Taulo za kike na Pampasi kwa ajili ya watoto.

Aidha Mbunge huyo alimkabidhi mkuu wa gereza shilingi laki mbili kwa ajili ya kununua nguo za wafungwa wa kike, huku akiahidi kupeleka katika gereza hilo magodoro na kuweka Tiles.

Mbunge Yustina Rahhi  alimbatana na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Manyara Fatuma Hassan, Mwenyekiti UWT mjini Babati Eva Luoga, Katibu UWT Babati mjini Zainabu Dodo, wajumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Babati mjini Modesta John, Paskalina Matata, Janeth Kadege, Amina Cherepa  na katibu Mwenezi Babati mjini  Salome Masasi.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Manyara Yustina Rahii na viongozi mbalimbali wa umoja wa wanawake (UWT) mkoa na wilaya ya Babati mjini.Share To:

Post A Comment: