Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile akiongea na wananchi wa Jimbo la Nachingwea katika kata ya Nachingwea akiwaeleza namna anavyofanya kazi kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo hilo.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya kimaendeleo katika Jimbo hilo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Nachingwea mbunge huyo alisema kuwa toka Rais Dr Samia suluhu Hassan aingie madarakani amepeleka fedha nyingi kwenye sekta ya barabara na kuifanya Nachingwea kuwa na taa kila kona ya mjini jambo ambalo kwa miaka mingi lilishindikana na kufanya mji huo kuwa kama miji mingine ya Tanzania.

Dr Chinguile alisema kuwa ICU Bora Tanzania imejengwa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea ambayo fedha zote za ujenzi wa hospitali hiyo zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan.

Alisema kuwa wakulima wa zao la korosho msimu huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan ametoa pembejeo za kilimo bure kwa wakulima wote wa Jimbo la Nachingwea na kuwapa furaha wananchi wote.

Aidha mbunge huyo alisema kuwa amewapunguzia usumbufu wa kuchangia ujenzi wa vyumba ya madarasa na nyumba za walimu Kwa kuweza kujenga majengo hayo kila mwaka na kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile alimazia kwa kumpongeza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mhandisi Chionda Kawawa Kwa kazi kubwa wanayoifanya kuijenga wilaya hiyo kimaendeleo na kiuchumi.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: