Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Mwantum Mgonja


Na Mwandishi Wetu 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Mwantum Mgonja ameipongeza kampuni ya Mainstream Media Limited kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika mkoa wa Kigoma.Pongezi hizo zimetolewa baada ya kampuni hiyo kuanzisha kituo che redio cha Main Fm 91.7 ambayo kimelenga kutoa habari na taarifa katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayofanywa ndani ya mkoa wa Kigoma  Bi. Mwantum ameyasema hayo wakati wa mahojiano katika studio za Main Fm kwenye tukio la kuwasha kipaza sauti (mic) kwa mara ya kwanza.Mkurugenzi huyo alisema serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya manispaa ya Kigoma Ujiji katika sekta mbalimbali hususani afya na elimu na pia akaongeza kusema redio hiyo itasaidia kutoa taarifa za aina hiyo kwa umma huku akishukuru kwa kupata fursa ya kuw wa kwanza kukizindua kito hicho. 

 Aidha mkurugenzi huyo pia alipata fursa ya kutoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali ambapo alisema kuwa mfuko wa maendeleo ya vijana unafanyiwa marekebisho na kuwataka vijana wa Mkoa wa Kigoma kuendelee kusikiliza vyombo vya habari hususani Main fm 91.7 kwa ajili ya kujua fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma ikiwemo mikopo nafuu inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi.

Mwantum aliambatana na diwani viti maalum kata ya Mwanga Kusini,mtendaji wa kata ya Mwanga Kusini na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kilimahewa pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Kigoma.Zoezi hili ya Kuwasha Kipaaza sauti (Mic) kwa mara ya kwanza lilifanyika Tarehe 10 Julai 2023.  Mainstream Media Limited, pamoja na uwekezaji huo pia wametoa fursa za ajira kwa Watangazaji na wadau wa tasnia ya habari kutoka maeneo mbali mbali hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kituo chao hicho kinafikisha ujumbe kwa urahisi na haraka zaidi kote duniani. Zoezi la kuwasha Vipaaza sauti (Mic) lilienda sambamba na kuwaruhusu wasikilizaji wa redio hii duniani kote kuisikiliza kupitia kwenye Masafa ya 91.7 FM Kigoma na kupitia kwenye tovuti ya Main FM (www.mainfm.co.tz Pia Meneja wa kituo Bw. Felician hulilo, alisema kuwa Main FM imeanzia Kigoma lakini menejimenti yake imelenga kuipeleka redio hii katika mikoa yote ya Tanzania. 

Share To:

Post A Comment: