Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC chini ya Ushirikiano wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wanayodhamira kubwa ya kuweza kuleta mapinduzi ya utalii wa mikutano,kwa kujenga kituo kikubwa kitakachoitwa Mount Kilimanjaro International Convention Center (MKICC)kitakachokuwa na ukumbi wenye ukubwa wa kubeba wageni 3000, eneo la maonyesho lenye uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 10,000 pamoja na eneo watakalowekeza hoteli za Kitalii.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa AICC Efraim Mafuru amesema tayari wanalo eneo Site D1 la heka 90 zenye umbali wa kilometa 2 amesema lengo lao ni kulibadilisha matumizi na wataanza kwa kujenga hoteli moja ya nyota tano,japo mpango wao ni kuwa na hoteli mbili za nyota tano zenye uwezo wa kuchukua wageni zaidi ya 1000,ambapo wataanza ujenzi mwaka huu wa fedha.

‘’Tutaendelea kuwekeza katika kumbi kubwa za kisasa ili Tanzania iweze kushindana ,sasa hivi kama mnavyojua tulikuwa wa 11 katika Afrika miaka 4 iliyopita lakini ndani ya miaka 2ya uongozi wa serikali ya awamu ya 6 Tanzania imepanda hadi nafasi ya 5,lakini mimi nasema dhamira yetu ni kuingia tatu bora ndani ya muda mfupi’’Alisema Mafuru

Mafuru amesema kuwa kwa kuzingatia mchango wa Economic Diplomacy ili kuweza kuwaleta wadau waliopo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii wa mkutano watawekeza pia katika shopping Mall kubwa ili wafanya biashara waweze kuja kuuza bidhaa zao kwa wageni wanaokuja katika mikutano

‘’Mbali na hivyo tunaamini kwamba ili kuweza kuwahudumia viongozi wakuu wan chi tutaweka maeneo maalum ambayo tutatoa taarifa baadae yatakavyokuwa lakini hata tukiweza kuwa na viongozi zaidi ya 15-20 kwa kwa wakati mmoja tuweze kuwahudumia,na kutimiza dhamira na ndoto ya Mhe.Samia Suluhu ya ya kufanya Tanzania kitovu cha utalii wa mikutano itatekelezwa katika kiwanja hiki’’Alisema Mafuru.

Kwa upande wake msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa aliipongeza AICC kwa mapango wao huo na kusema Serikali inautazama mkoa wa Arusha kama mkoa wa kimkakati na Kwenda na ndoto yake ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii Barani Afrika na inahitaji mchango mkubwa na sauti ya pamoja kutoka kwa wadau

‘’kumekuwa na tabia Fulani kwamba mambo makubwa na mipango kama hii inapotaka kufanyika kuna vikundi vya watu vinatengeneza fitna ,hebu tuache fitna mafanikio yoyote ya kiuchumi yanataka uwekezaji,na lazima ushirikiane na sekta binafsi,kwahiyo watanzania mtuelewe kwasababu tunataka makusanyo ya mapato yanayotumika naserikali tuyatumie Kwenda kutoa huduma kwa watanzania ,mfano uwekezaji wa kituo kikubwa cha uwekezaji ni biashara’’Alisema Msigwa.

Msigwa amesema ilani ya CCM imewaelekeza kufikia watalii mil 5 ifikapo mwaka 2025,ambapo kwa sasa wameanza Kwenda vyema mwaka 2022 waliweza kufikia watalii mil 1.5,ambapo wanaweza kufikia watalii mil 2kwa kipindi kifupi kijacho kwani safari bado inaendelea kwaajili ya kufikia idadi hiyo ya wageni.

Amewataka Watanzania kuelewa kwamba wanapokwenda kwenye uwekezaji mkubwa kama huo Serikali inaangalia kwa karibu na kuangalia maslahi ya Taifa,ukiangalia mwaka 2022 AICC wameingiza mapato ya Bil 17 ,ambapo wanasema wakiwekeza wanaweza kufikia hadi bil 40-100

‘’Tutoke kwenye mapato madogo tunayoyapata twende kwenye mapato makubwa kwa kutumia style za kisasa za uwekezaji na haya mambo yanawezekana,lazima tuingize mawazo mapya yanayokuja kutuletea mageuzi na maendeleo’’Alisema Msigwa.
Share To:

Post A Comment: