Wajumbe zaidi ya 500 wa mkutano wa mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT wamehitismisha mkutano wao wa 38 kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro Mkoani Arusha.


Wakiwa katika ziara hiyo Kaimu katibu mkuu wa ALAT, Mohamed Majijd  ameeleza kuwa ujumbe huo unaojumuisha  Majiji, Manispaa na Halmashauri 184 kwa umoja wao baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha wameamua kumuunga  mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea vivutio va utalii vilivyoko katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ili wanaporudi kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.

“Kama watu kutoka nchi za Ulaya, Amerika, Asia wanakuja hadi Ngorongoro kutembelea vivutio vyetu, na Mhe. Rais ameshaonyesha njia, sisi kama viongozi katika maeneo yetu tunapaswa kuiga na kuonyesha mfano kwa wananchi wetu na ndio maana tukaona baada ya mkutano wetu wa mwaka  tuje kutembelea Ngorongoro na kuenzi Juhudi za Mhe. Rais kuona vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro na tuweze kuvitangaza kwa nguvu tukakavyorudi kwenye maeneo yetu ya Mikoa” amefafanua mhe Majjid.

Mjumbe wa ALAT Taifa ambae ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Jafari Naigesha ameeleza kuwa ujumbe  ziara ya viongozi hao kutembelea Ngorongoro imeamsha ari kwa viongozi wengi kwa kuwa wengi wao ni mara ya kwanza kutembelea hifadhi hiyo na kuongeza kuwa wanajipanga kuleta familia, makundi mbalimbali ya watumishi na wananchi kutoka halmashauri zao ili kuja wakati wa sikukuu na likizo kushugudia utajiri wa vivutio vilivyoko hifadhi ya Ngorongoro.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Dkt. Juma Mhina amebainisha kuwa katika ziara hiyo wajumbe hao wameona vivutio mbalimbali ikiwemo Kreta ya Ngorongoro,  vivutio vya aina za Wanyama mbalimbali ikiwemo Wanyama wakubwa watano (Big 5),  uoto wa mazingira asilia, msitu wa nyanda za juu kaskazini ambao ni makazi ya Wanyama wakubwa kama Tembo, Nyati Faru , chui, simba na wengine wengi.

Ameongeza kuwa vivutio vya utalii vinavyopatikana Mkoa wa Arusha na kanda ya kaskazini kwa ujumla vinachangia zaidi ya asilimia 75 ya mapato ya utalii Nchini hivyo wao kama viongozi wameona haja ya kuchangia mapato hayo kwa kulipa viingilio wa watu na magari ya wageni takribani 75 katika hifadhi ya Ngorongoro.

Akizungumza na Ujumbe huo Afisa Uhifadhi amkuu ambaye ni meneja Kitengo cha Uhusiano wa Umma NCAA Joyce Mgaya ujio wa viongozi na wajumbe wa ALAT Taifa ni muendelezo wa hifadhi ya Ngorongoro kupokea makundi mbalimbali ya wageni ambayo yameongeza idadi ya wageni kufikia zaidi ya laki 7 mwaka 2018/2019 na kwa mwaka 2022/2023 NCAA inategemea kupokea wageni kati ya 1,000,000 hadi 1,500,000.

Kwa upande wake Meneja wa huduma za Utalii NCAA Peter Makutian ameeleza ujumbe huo kuwa hifadhi ya Ngorongoro yenye vivutio vingi vya utalii ilianzishwa mwaka 1959.

Ametaja vivutio hivyo kuwa ni pamoja na  kreta kubwa tatu za Ngorongoro, Empakaai, Olmoti, bonde la Olduvai Gorge lenye kumbukumbu ya binabadu aliyeishia miaka 3.6 iliyopita, Mlima Lolmalasin ambao ni mlima wa 3 nchini kwa urefu , Mchanga unaohama, Bonde la Olkarean ambapo ndege aina ya Volture wanazaliana, tambarare za ndutu, Nyayo la Laetoli, maporomoko ya maji Endoro.

Vivutio hivi kwa ujumla vimechangia eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kutambulika kama moja ya maajabu 7 barani Afrika na kutambuliwa na UNESCO kama eneo la urithi wa dunia.


Share To:

Post A Comment: