NA DENIS CHAMBI, TANGA,

Katika kuadhimisha mwendelezo wa wiki ya sayansi Afrika kituo cha sayansi cha  Stem park kilichopo katika halmashauri ya jiji la Tanga kimetoa mafunzo ya hisabati , teknolojia na uhandisi kwa wanafunzi zaidi ya 350 wa shule mbalimbali za msingi zilizopo jijini hapa  yakilenga hasa kuongeza ari kwa wanafunzi kupenda kujifunza masomo ya sayansi kwa malengo yao ya baadaye na kuja kulisaidia Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa stem park Max George amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho kimeweza kusaidia na kuongeza ari kwa wanafunzi wengi kupenda kujifunza masomo ya sayansi na hisabati hatua ambayo inaleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla juu ya  kile kinachoelezwa kuwa masomo hayo ni magumu.

Alisema kuwa wanafunzi hao wa shule za msingi ambao wamejitokeza na kupata bahati ya kujifunza technologia, uhandisi pamoja na hisabati ni mwanzo wa  juni 26 hadi 30, 2023 ambapo  kutakuwa na wanafunzi wa shule  za sekondari kutoka mikoa mbalimbali ambao watajifunza teknologia ya juu kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikipelekea na adha mbalimbali.

“Tumesherehekea wiki ya sayansi kwa Afrika na watoto 350 kutoka shule mbalimbali za msingi wanaopatikana hapa jijini Tanga wamejifunza juu ya maswala ya hisabati , uhandisi na techolojia  kwa vitendo na katika mwendelezo wa kuhakikisha vijana wanedelea kujifunza kwa vitendo zaidi tarehe 26 hadi 30 tutakuwa na vijana wa sekondari kutoka mikoa tofauti toafauti ya Tanzanzia na wao watatengeneza projekti ambayo itakwenda kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.” Alisema Max.

Kwa upande wake Dkt. Isaya Ipyana ambaye ni balozi wa Next Einstein Forum ambao ni waandaaji wa makongamano ya sayansi Afrika kwa wakishirikiana na Sperm Parka katika mkoa wa Tanga amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika sekta ya elimu ikiwemo miundombinu na mabadiliko ya sera ambapo ameiomba serikali kuzidi kuboresha sekta hiyo kwa kuongeza vifaa vya kujifunza na kujifunzi ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuelewa zaidi.

“Tunapongeza jitihada nzima za serikali kwa kuwa imekuwa ikifanya mabadiliko katika sera mbalimbali za  elimu lakini imekuwa inaruhusu wadau wanohusika na maswala ya elimu kufanya kazi katika mazingira mazuri kabisa sisi kama wadau tutaendelea kuhakikisha tunasonga mbele” alisema Dkt Ipiana.

Enistein Forum  kwa kushirikiana na kituo cha Stem Park kwa pamoja na  halmashauri ya jiji la Tanga june 23 imeandaa tuzo maalum ambazo watatunukiwa walimu wa kike wanaofanya vizuri katika masomo ya hesabu na sayansi hii ikilenga hasa kuongeza hamasa kwa walimu kuongeza molari ya kufanya kazi na wanafunzi kupenda na kuwa mabalozi kwa wengine juu ya  masomo ya sayansi na hisabati .

Meneja wa kituo cha sayansi cha Stem Park kilichopo jijini Tanga mkoani hapa Max George akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo wakati wakisherehekea wiki ya sayansi Afrika na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi leo. june 21,2023.

Balozi wa Next Eisteini  Forum( Waandaaji wa makongamano ya sayansi Afrika ) Dkt Isaya Ipiano akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya sayansi Afrika na ushiriki wao katika kituo cha Stem Park Tanga.

Mmoja wa walimu wa kituo cha Stem Park Tanga akiwaelekeza wanafunzi mfano wa muundo wa daraja lililotengenezwa ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya sayansi Afrika.






Share To:

Post A Comment: