Na Mapuli Misalaba

Baadhi ya viongozi wa kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wanatarajia kushirikia kwenye hafla ya SMAUJATA CHAMPIONS AWARDS ambayo itafanyika kitaifa kesho jijini Dodoma.

Hafla hiyo itaambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ambapo mashujaa wa SMAUJATA mikoa yote wanatarajiwa kuhudhuria na kwamba lengo ni kupongezana kwa kufikisha Mwaka mmoja wa kampeni hiyo ya kupinga na kutokomeza ukatili Nchini ambayo ilizinduliwa na waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima Juni 16,2022.

SMAUJATA ni kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili Nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka jana chini ya Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter Mosewe Bulugu

SMAUJATA inawakaribisha wananachi wote kuhudhuria hafla hiyo siku ya kesho Juni 16,2023 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi wa pili kutoka upande wa kushoto akiwa na baadhi ya viongozi baada ya kufika jijini Dodoma leo Juni 15,2023.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: