Mwandishi wetu-Mbulu

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP George Katabazi ametoa Rai kwa viongozi wa Dini mbalimbali wilayani Mbulu Mkoani Manyara kuendelea kufanya kazi ya mungu Kwa uaminifu,Uhodarina kwa moyo dhabiti ili kupunguza matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia na Matukio mengine.

Akizungumza akiwa wilayani Mbulu RPC Katabazi amesema viongozi wa Dini wananafasi ya kukabiliana na matukio hayo kwa kuiasa jamii na kuihudumia kiroho jambo litakalo saidia kupunguza matukio ya kiuhalifu ikiwemo Wizi,Ulawiti, Mauwaji,pamojana matumizi ya Dawa za Kulevya.

Aidha amesema Matukio Mengi ya kiuhalifu yanatokana na watu kukosa hofu ya Mungu,huku akizitaja Baadhi ya kata zinazoongoza kwa matukio mengi katika  wilaya ya Mbulu ikiwemo Kata ya Yaeda Chini,Bashay,Endagikoki,Haydom,Tumati,Tlaw, kuongezeka lwa Matukio hivyo na kusababisha matukio hayo kutokea.

Aidha ACP Katabazi amesema  Kuhusu Hali ya Ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa mkoa wa Manyara, kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita mpaka mei 2023 hali sio nzuri kwani Jumla ya kesi 148 ziliripotiwa huku katika wilaya ya Mbulu pekee zilifunguliwa Kesi 42, Wilaya ya Babati kesi 51, Hanang kesi 12, Simanjiro 32 na wilaya ya Kiteto Kesi 11.

Kwa upande wao viongozi wa Dini wamepongeza hatuwa hiyo ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ya kufanya ziara na kukutana na Makundi Mbalombali Kwani itasadia pakubwa katika kuongeza ushirikiano Baina ya jeshi hilo la polisi  na Viongozi wa Dini katika mkoa wa Manyara na kushirikiana katika kupunguza Matukio ya ukatili wa kijinsia.

Share To:

Post A Comment: