MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde anatarajia kuanzisha mashindano makubwa ya michezo kwa wanafunzi wa shule za Sekondari jijini Dodoma.
Lengo la mashindano hayo ni  kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa jiji hilo.
Akizungumza na HabariLEO, Mavunde amesema kuanzia mwakani 2024, ataanzisha  mashindano makubwa ya michezo mbalimbali kwa kushirikisha shule zote za jijini la Dodoma kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana.
Aidha, amesema anashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa kuanza ujenzi wa vituo vya michezo Jljijini hapo   ambapo wanafunzi wengi watapata nafasi ya kuweza kuvitumia na kukuza vipaji vyao.
Wakati huo huo, Mavunde amemkabidhi
 vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh milioni  4  kwa wanafunzi wanamichezo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambao wanashiriki mashindano ya michezo ya Shule za Sekondari(UMISSETA) katika ngazi ya Mkoa.
Awali, Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma  Zainab Abdallah Mohamed alimshukuru Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa na mchango mkubwa kukuza michezo katika shule za Sekondari Jijini Dodoma na kuahidi kwamba watafanya vizuri katika mashindano ya UMISSETA ngazi ya mkoa na kuliwakilisha vyema Jiji la Dodoma.
Share To:

Post A Comment: