NA DENIS CHAMBI, TANGA.

MAMLAKA ya Usimamizi wa bandari 'TPA' Tanga imeibuka  kuwa mshindi wa  jumla katika maonyesho ya biashara na utalii  yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga kwa mwaka 2023 yaliyoandaliwa na chemba ya biashara'


Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Tanga yakihusisha taasisi, kampuni na mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi sambamba na wafanyabiashara mbalimbali wakitangaza biashara zao.

Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba June 6,2023  kaimu meneja wa mamlaka ya Bandari Tanga Petter Milanzi alisema kuwa wamekuja kivingine katika utoaji wa huduma bora kwa wadau na wafanya biashara wote wa ndani na nje ya nchi wanapotumia bandari hiyo.

"Tanga sasa ni lango kuu la uchumi wa afrika mashariki na sisi tunasema bandari ni lango la biashara kitaifa na kimataifa na tumekuja katika maonyesho ya biashara na utalii kuwahakikishia wateja wetu kwamba wafike na waitumie bandari yetu ya Tanga na sisi tutawapa huduma bora  ambazo wanazitarajia katika viwango vya kimataifa"

"Sasa hivi bandari ya Tanga imezaliwa upya maana yake sisi sasa mambo mengi tunayafanya kimataifa na ndio maana tumekuwa  washiriki wa kwanza katika vipengele vyote vilivyoshindanishwa  katika maonyesho ya biashara na utalii kwa mwaka 2023 na tulikuwa wafadhili wakubwa  ili kuhakikisha  maonyesho haya yanafanyika kwa ufanisi zaidi" alisema Milanzi.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha masoko katika bandari hiyo  Rose Tandiko  ambao pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 2013 alisema kuwa wameyatumia vyema kwa kuwapa elimu washiriki na wadau mbalimbali waliojitokeza ambapo  wameongeza wigo mpana kwa watumiaji wa bandari hiyo.

"Bandari ya Tanga sasa imekuwa mpya vifaa vimeongezwa vimekuwa vingi ari ya utendaji kwa wafanyakazi wa bandari ya Tanga imeongezeka kwa kiwango cha juu zaidi na wako tayari kuhudumia meli za aina yoyote na mizigo yeyote  kwa sababu vifaa vipo tumewezeshwa na serikali" alisema Tandiko  

"Ukiacha kutoa elimu kwa wale ambao hawafahamu kazi zetu tumeweza kukutana na wadau wengi ambao tunafanya nao kazi kupitia bandari tuweza kupata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwao na sisi tumepokea maoni yao   kwaajili kwenda  kuboresha utendaji kazi wetu" alisema Tandiko.

Bandari ya Tanga  ambayo imefanyiwa maboresho makubwa kwa upanuzi wa kina cha bahari na ukarabatI wa gati mbili kupitia fedha zilizo wekezwa na serikali  zaidi ya billion 400 na kuwezesha meli kubwa kutoka nchi mbalimbali kushusha mizigo na kupakia bandarini hapo tofauti na miaka ya nyuma.
Kaimu meneja wa mamlaka ya bandari Tanga Petter Milanzi pamoja na wafanyakazi wa mamlaka hiyo mara baada ya kutangazwa kuwa wahindi wa jumla katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba  (kushoto) akimkabidhi Kaimu meneja wa Bandari ta Tanga Petter Milanzi   baada ya kuibuka kuwa washindi wa jumla kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yaliyomalizika june 6 katika viwanja vya Mwahako.
 


Share To:

Post A Comment: