Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Saitoti Stephen Zelothe kuwasilishe taarifa kila baada ya siku mbili juu ya maendeleo ya makusanyo ya mapato.

"Nataka kasi ya ukusanyaji wa mapato inaongezeka kutoka asilimia 72 ya sasa mpaka kufikia asilimia 100 ndani wa wiki mbili zilizobaki kabla ya kufunga mwaka wa fedha 2021/2022" amesisitiza zaidi Kindamba.

Kindamba ametoa maelekezo hayo kwenye kikao cha Baraza maaalum la madiwani cha kujadili na kupitia hoja za Mkaguzi wa ndani wa hesabu za Serikali (CAG) katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 mjini Songe Wilayani Kilindi.

Amesema kupitia taarifa hizo Timu ya Wataalamu itaweza kutoa ushauri wao wa nini kinaweza kufanyika ili kufikia malengo ya Serikali katika ukusanyi wa mapato katika Halmashauri hiyo

Aidha Kindamba amewataka Wakuu wa Idara na Wataalamu kwa kushirikiana na Baraza la Madiwani kumsaidia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu ili kuepukana na Hoja za Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Naye Katibu Tawala mkoa wa Tanga Pili Mnyema amesema licha ya Halmashauri hiyo kuwa na rasilimali za kutosha kama Madini na Vito mbali mbaki bado Halmashauri haijanuifaika kupitia Sekta hiyo, ambapo amewataka kuitumia Vizuri Sekta ya Madini ili kubadilisha maisha ya wananchi.
Share To:

Post A Comment: