Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na waandishi wa habari kuhusu agizo la MANAWASA kulipa zaidi million 113 wanazodaiwa na TANESCO Wilaya ya Nachingwea

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.



MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametoa siku Saba kwa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) kulipa zaidi million 113 wanazodaiwa na TANESCO Wilaya ya Nachingwea ili  kurejesha huduma ya maji kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa MANAWASA wanatakiwa kurudisha haraka iwezekanavyo huduma ya maji kwa wananchi kutokana uzembe wao kushindwa kulipa bill za umeme kwa TANESCO.

Moyo alisema kuwa Mamlaka hiyo imekuwa na wafanyakazi wazembe ambao wameshindwa kudai madeni Kwa wateja ambao wanaowadai hadi kusababisha huduma ya maji kukatika Kwa wateja ambao hawadaiwi bili za maji.

Alisema haiwezekani MANAWASA wanadai zaidi ya million 130 kwa wateja wao na wanashindwa kuzikusanya Kwa wakati hadi TANESCO wanaamua kuwakatika umeme na kusababisha adha kubwa Kwa wananchi kukosa maji safi na salama 

Moyo aliagiza taasisi zote za serikali,binafsi na wananchi wanazodaiwa bili ya maji na MANAWASA ili kuisaidia Mamlaka hiyo kuendesha shughuli zao kiufanisi.


Alimazia kwa kuwataka TANESCO kurudisha umeme mara Moja kwa MANAWASA ili shughuli ya utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi iendelee kama awali huku taasisi hizo mbili zikiendelea na majadiliano mezani.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: