NA DENIS CHAMBI,TANGA
WAKALA wa usajili wa biashara na leseni ‘BRELA’ imewataka wafanyabishara wote wakubwa, wakati na wadogo waliopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kurasimisha biashara zao ili kuweza kuchangia pato la Taifa ambapo pia itawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.
Rai
hiyo ometolewa na afisa leseni kutoka BRELA Jubilate Muro wakati
akizungumza na wanahabari katika maonyesho ya 10 ya biashara na viweanda
yanayofanyika mkoani Tanga ambapo amesma kuwa wapo wafanyabishara wengi
wanaofanya biashara wakiwa hawajarasimisha jambo ambalo ni kinyume cha
sheria zilizopo ili kujenga uaminifu kwa wateja na wafanyabishara
wengine
"Tunawaomba sana
wafanyabishara wote nchini wasajili biashara zao kwasababu kuna faida
kubwa kwa kufanya hivyo kuliko kutokusajili a lakini pia kuna huduma
zingine mfanyabishara ,mmiliki wa kiwanda au kampuni atashindwa kuzipata
kwa kukwepa kusajili biashara yake kupitia BRELA"
“Lakini
hii pia itamsaidia kujenga uaminifu kwa wateja wake na wafanyabishara
wengine na hata kwenye taasisi za kifedha ataweza kuhudumiwa kama
atahitaji mkopo akiwa na leseni ya kibiahara vinginevyo anaweza kukosa
huduma muhimu ambazo zinaweza kumleta maendeleo”
alisema Muro.
Maonyesho
ya biashara na utalii ambayo hufanyika kila mwaka jijini Tanga
yakihusisha makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
mwaka huu yakiwa ni ya 10 yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda
utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’
Kwa
upande wake afisa usajili kutoka BRELA Julieth Kihwelu alisema kuwa
mifumo hiyo ni mikuu pendwa ambayo mwombaji anatakiwa kutumia
kuwasilisha ombi lake huku akieleza wanatoa huduma ya kuwafundisha namna
ya kutumia mfumo huo kuweza kujisajili.
“Katika
mifumo hii mwombaji anatakiwa awe na kitambulisho na Taifa,barua pepe
aweze kujisaijili na nitoe wito kwa wajasiriamali nchini kuendelea
kusajili alama za biashara zao kwa kuwa alama moja inamtumbisla mtu
mmoja”Alisema
Hata hivyo
aliwashauri wakazi wa Tanga na mikoa ya jirani waenda kupata huduma ya
papo kwa papo ambapo kwa sasa wanaendelea kutoa huduma hiyo katika
maeneo hayo.
“Tokea 28
mei mpaka Mei 31 tumekwisha kuwahudumia wananchi 35 na tukilinganisha
mwaka jana na mwaka huu kuna utofauti na tunategemea kufikia watu wengi
kwa kuwatembele kwenye mabanda hususani wajasiriamali kuweza kuwapa
ushauri namna ya kuweza kusajili alama za biashara “Alisema Afisa huyo.
Afisa leseni kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni ‘BRELA’ Jubilae Muro akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya mwahako mkoani Tanga.
Wafanyakazi kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni ‘BRELA’ wakitoa huduma na elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya mwahako Mkoani Tanga.
Wafanyakazi kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni ‘BRELA’ wakitoa huduma na elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya mwahako Mkoani Tanga.
Post A Comment: