Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed Mussa, amekipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kufundisha kozi ambazo zinalenga kutatua changamogo mbalimbali katika jamii.

Mhe. Lela amesema hayo leo alipotembelea banda la Chuo katika Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi - NACTVET yanayoendelea Jijini Arusha.


Mhe. Lela pia amekipongeza Chuo kwa kuendeleza uzalendo na kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa taifa hili  kwa kutoa majina ya waasisi wa Taifa kwa chuo na kampasi zake.

" Chuo hiki kina majina ya Wasisi wa Taifa ambao ni baba wa Taifa Mwalimu Jullius Kambarage Nyerere na Sheikh Amri Abeid Karume  alisisitiza Mhe. Waziri Lela.


Aidha, Waziri amekipongeza Chuo kwa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za Kitaifa hususan kwa upande wa Kampasi ya Karume - Zanzibar.


Imetolewa na:


Kitengo Cha Habari na Masoko.

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

20.05.2023

Share To:

Post A Comment: