Serikali imewataka wananchi Wilayani Tarime Mkoani Mara kuheshimu maeneo ya Hifadhi kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary  Masanja (Mb) amesema hayo Mei 6,2023 katika kijiji cha Gibaso Kata ya Kwihancha wakati wa ziara ya Mawaziri Watatu kutoka  Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja  na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya  Serengeti. 

Amesema kuwa mwananchi yeyote haruhusiwi kukanyaga hifadhini, kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali na changamoto za majangili

"Nimesikia hapa kuna malalamiko mengi pindi mnapoingia ndani ya Hifadhi, Naomba kuwaeleza kuwa 

eneo lile linatunzwa kwa sheria za nchi na hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kibinadamu" Mhe. Masanja amesisitiza. 

Aidha, amefafanua kuwa kazi ya Askari wa Uhifadhi walio katika maeneo ya Hifadhi ni kulinda Hifadhi pamoja na rasilimali zilizomo hifadhini na si vinginevyo.

Amewaasa wananchi hao kuacha tabia ya kuwalaumu Askari Uhifadhi na badala yake waheshimu sheria za nchi kwa kuacha kuingia katika maeneo hayo

Mhe. Masanja amewataka wananchi kukaa katika maeneo ya vijiji yanayoruhusiwa kwa shughuli za kibinadamu. 

"Kaeni kwenye maeneo yanayoruhusiwa yaacheni maeneo ya hifadhi yahifadhiwe  na wataalamu waliokasimiwa madaraka na Serikali" Mhe. Masanja amesema.

Share To:

Post A Comment: