NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imeondolewa kwenye hatua ya nusu fainali na Azam Fc kwa kupokea  kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo huo  ambao uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda mkoani Mtwara.

Katika Mchezo huo Azam Fc walianza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa mlinzi wao wa kulia Lusajo Mwaikenda kabla ya Simba kusawazisha kupitia kwa Sadio Kanout dakika ya 28 ya mchezo na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili Azam Fc waliingia uwanjani kwa kushambulia zaidi kwani walitengeneza nafasi nyingi za magoli bila mafaniko.

Azam Fc ilifanya mabadiliko kwa baadhiya wachezaji wao ambapo mbadiliko yalizaa matunda kwani alitoka Idris Mbombo na nafasi yake kuchukuliwa na Prince Dube ambaye alipachika bao kali ambalo liliwapa matokeo ya ushindi wa 2-1 na kutinga hatua ya Fainali ambayo itapigwa kwenye dimba la Mkwakwani Tanga.

Share To:

Post A Comment: