Mkuu wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema kila Kozi inayotolewa Chuoni hapo ndani yake inaambatana na mafunzo ya uongozi, Madili na Uzalendo.

Prof. Mwakalila amesema hayo leo alipotembelea banda la Chuo katika Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi- NACTVET yanayoendelea jijini Arusha.


Mkuu huyo wa Chuo amesema ni fursa kwa Chuo kushiriki Maonesho hayo kwa kuwa inatoa nafasi kwa Wananchi na Wadau kuona na kujifunza kuhusu bunifu mbalimbali zinazokuwa zinaoneshwa na Wanafunzi wa chuo hicho.

Amesema kozi za Chuo zimekuwa na tija, hivyo imechangia kwa Chuo kuwa na ongezeko la wanafunzi.

Kuhusu Miundombinu ya chuo Profesa Mwakalila amessma Chuo kina mazingira mazuri na rafiki kwa kujifunzia na kufundishia kwa kampasi zote ikiwemo ile ya Kivukoni - Dar es salaam, Karume- Zanzibar na Kampasi ya Pemba.


Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayofanyika jijini Arusha yameanza tarehe Mei 16, 2023 na yatakamilika Mei 22, 2023 na kauli mbiu yake ni Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Nguvu kazi Mahiri.


Imetolewa na kitengo cha Habari na Masoko

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

19.05.2023

Share To:

Post A Comment: