Na Okuly Julius-Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson amelipongeza Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kuendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi wake kwa kufikisha huduma haraka kwa wateja wao.


Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.



Aidha Spika amelitaka shirika hilo kujipambanua kwa kuongeza nguvu zaidi kwa kuwa limeweshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani za makazi hivyo inakuwa rahisi kwao kufikisha huduma haraka Kwa wateja wao.


Dkt.Tulia amesema kuwepo Kwa mfumo wa anuani za makazi kunasaidia Kwa kiasi kikubwa Shirika hilo ,kuwafikia wateja endapo mteja atakuwa amesajili makazi yake hivyo kumuwezesha mtoa huduma wa Posta kufahamu Kwa haraka namba ya nyumba, jina la mtaa au Barabara, pindi anapopeleka mzigo Kwa mteja wake hivyo ni vyema kuongeza nguvu zaidi.


"Shirika letu la Posta sasa nafikiri mjipambanue zaidi Kwa sababu mmewezeshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani ya makazi ukimutumia mtu barua inaenda hadi nyumbani kwake kwakuwa tayari namba ya nyumba yake inafahamika hivyo ongezeni nguvu''amesema


Hata hivyo amewataka wananchi ambao hawajasajili makazi yao kusajili Kwani mtu kujua anuani yake ya makazi zinasaidia kupata huduma Kwa haraka na kuchochea maendeleo



Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Elia Madulesi, amesema kuwa Kwa sasa mwananchi anafikiwa Kwa urahisi na huduma za Shirika la Posta Tanzania kutokana na kukamilika Kwa Mradi wa Anuani za makazi ambayo Kwa sasa huduma ya vifurushi,vipeto na barua bila kupotezewa Muda.


"Siyo hivyo tu Kwa sasa Mteja wa POSTA anaona kabisa mzigo wake Jinsia unavyosafirishwa Kwa kutumia mtandao hivyo tumekuwa kidijitali zaidi na baada ya hapo mzigo utamfikia mlengwa Kwa wakati kwani Anuani za makazi zimerahisisha Kila kitu,"


Na kuongeza kuwa "Shirika la Posta na Anuani za Makazi ni mapecha Kwa sababu tangu kuimarishwa Kwa mfumo huu wa Anuani za Makazi mambo yamekuwa rahisi sana na huduma imekuwa na ufanisi,"amesema Madulesi


Madulesi,amesema tangu Anuani za Makazi kukamilike Shirika la Posta limeongeza usambazaja wa vipeto,barua na vifurushi Kwa asilimia 14.


Maonesho ya wadau wa Mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano iliyosomwa leo na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: