Na John Walter- Manyara

Kwa kipindi cha Januari 2023 hadi Machi 2023 Katika mkoa wa Manyara yameripotiwa matukio 2,000 ya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari na Kongamano la kupinga Ukatili wa Kijinsia leo Mei 9,2023 Mjini Babati, Afisa Maendeleo ya jamii mkoani hapa Lilian Bajune amesema vitendo vingine vya Ukatili vinafanyika ndani ya familia.

Kati ya matukio hayo, 187 Ukatili wa Kiuchumi,285 Ukatili wa Kingono,944 Ukatili wa kimwili na Matukio 931 Ukatili wa kihisia.

Katibu tawala Mkoa wa Manyara Karolina Mthapula amesema mkoa unaendelea na hatua mbalimbali ikiwemo kutoa elimu Kwa jamii.

Mwanasheria kutoka Civil Social Protection foundation (CSP) Eliakim Paulo amesema matukio ya Ukatili mara nyingi yanashindwa kuchuliwa hatua kutokana na kukosa ushahidi.

Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Mkoa wa Manyara Maarufu Mkwaya amepongeza juhudi zinazofanywa na wadau katika kutokomeza Ukatili wakiwemo waandishi wa Habari.

Viongozi wa dini mbalimbali mkoa wa Manyara wamesema ni wakati wa Serikali kuweka maazimio kwa kushirikisha wadau ili kutafuta njia ya kutatua tatizo.

Waandishi wa Habari wameahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii kupitia vyombo vyao juu ya madhara ya Ukatili wa Kijinsia na kuacha Imani potofu.
Share To:

Post A Comment: