Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewasihi wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuwafundisha watoto kutoa taarifa za viashiria vya ukatili na uharifu ambao wanakutana nao.

Ameyasema hayo kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la Investing in Children and Societies (ICS) ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo walimu walezi pamoja na wanafunzi wajumbe wa baraza la watoto Wilaya ya Shinyanga ili kupunguza au kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mstahiki meya pamoja na mambo mengine amewakumbusha wawezeshaji katika mafunzo hayo kuona namna bora ya kutoa elimu kwenye familia ili kutambua umuhimu katika malezi ya watoto ili kuepukana na vitendo vya ukatili unaoendelea kufanyika.

Mhe. Masumbuka amesisitiza wazazi, walezi pamoja na wadau mbalimbali ambao wanatetea haki za watoto kuendelea kutoa elimu kwa kuwafundisha watoto kutoa taarifa za viashiria vya ukatili na ukatili wanaofanyiwa ili kutokomeza vitendo hivyo.

Amesema ni muhimu kuwafundisha watoto madhara yanayotokana  na vitendo vya ukatili ili kukua katika mazingira salama ya kuishi huku akiwaomba wananchi kuhudhuria kwenye nyumba za ibada ili kujengewa ufahamu zaidi katika kuepuka uovu.

“Kama unaona kuna tukio siyo la kawaida popote pale toa taarifa wafundisheni watoto kutoa taarifa, ukatili na uhalifu utaisha tukitoa taarifa toa taarifa badala ya kunyamaza na kusema hayakuhusu nanyi walezi myaishi hayo mnayoyafundisha” ameongeza Mhe. Masumbuko.

“Siku hizi tumekuwa na watoto wasio na adabu, vijana wasio na adabu lakini pia wazee wasio na adabu kutokana na mambo kadhaa ukiwemo utandawazi unakuta wazazi hawaelewani, wanagombana mbele ya watoto, hali hii inasababisha watoto wetu waige tabia za ajabu , wasiwe salama nidhamu ya watoto inatakiwa ianzie ndani ya familia ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama muda wote”,ameeleza Mh. Masumbuko.

“Tuwe wabunifu ili watoto wetu wawe salama, tuwe wawazi tuwaeleze watoto ukweli kuhusu madhara ya matendo ya hovyo tuhakikishe tunasimamia mafundisho sahihi na maadili mema ili watoto wetu wawe salama na jamii iepukane na vitendo vya ukatili wa kijinsia na maovu kama vile ushoga na usagaji”,amesema Mhe. Masumbuko.

Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Divisheni ya Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea ameelezea mafunzo hayo huku akisema matarajio baada ya walimu hao na wanafunzi kupata elimu juu ya ukatili.

Amesema maratajio baada ya mafunzo hayo ni walimu kwenda kufanya mabadiliko chanya kwa kubaini wote wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ama watoto ambao wapo kwenye mazingira hatarishi.

Aidha amewaomba wazazi na walezi kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao ili kubaini changamoto zinazowakabili hasa wawapo shuleni.

“Watoto wengi wanakuwa katika mazingira hatarishi kutokana na wazazi kuwa na shughuli nyingi ‘Busy’, kutojali na kutotenga muda wa kuongea na watoto walimu ni wachache wameachiwa mzigo wa kulea wanafunzi wengi, wanaelemewa hivyo wazazi wanatakiwa kushirikiana na walimu na majirani kulea watoto lakini ni lazima wazazi wajitahidi kuwajua marafiki wa watoto wao”,amesema Mbonea.

“Tuendelee pia kuhamasishana kuhusu kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari ili kuepusha na vishawishi wanavyokutana navyo watoto wawapo njiani kwenda au kutoka shuleni”, amesema.

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Investing in Children and Societies (ICS) wameendesha mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo yameanza  Jumanne Mei 16,2023  na yamehitimishwa leo Mei 17,2023 katika ukumbi wa Mama wa Mama Samia uliopo shule ya Msingi Buhangija mjini  Shinyanga.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga yakiendelea katika ukumbi wa Mama Samia uliopo shule ya Buhangija mjini Shinyanga.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: