MBULU


Mkuu wa Wilaya  ya Mbulu Komred Kheri James, Mapema Leo ametembelea Kata ya Murray iliopo katika Halimashauri ya Mbulu Mji kwa Lengo la Kuzungumza na Viongozi na Wananchi Baada ya Matukio Mawili ya Mauji yalio tokea na kupelekea vifo vya Watu Watatu  ambao ni Marehemu SAFARI AWE Mwenye Umri wa Miaka 55, aliefariki  kwa Kupigwa hadi Kufa na Mtoto wa Kaka yake alie Fahamika kwa jina la PETRO PAULO BAHA Mwenye Umri wa Miaka 22, ambae pia ali uawa na Wananchi baada ya Kuumuua Baba yake Mdogo katika Kitongoji cha Tseita.

Tukio la Tatu ni Mauji ya Mtoto Tumaini Paulo mwenye umri wa miaka 10, Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza alie uliwa na Baba Yake Wakufikia anaefahamika kwa Jina la PETRO JOHN ambae anashikiliwa na Jeshi la Polisi ili aweze kufikishwa Mahakamani.      

Akizungumza katika mkutano huo Komred Kheri James amelaani vikali matendo ya watu kujichukulia sheria mkononi bila  kufuata misingi ya utawala wa sheria na utoaji wa taarifa katika vyombo vyenye dhamana ya usimamizi wa usalama na utoaji wa Haki.                   

Akizungumza na wananchi na viongozi katika kikao hicho, Komred Kheri James kaeleza kuwa ni kosa kwa Mwananchi Yoyote au Kikundi Kujichukulia Mamlaka ya Kutuhumu na Kuhukumu bila Kushirikisha Mamlaka zinazo Husika.                         

Baadhi ya Mambo yaliotajwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James Kama Vyanzo Vikuu vya Matukio ya Mauji katika baadhi ya Maeneo ya Wilaya ya Mbulu ni; Ukatili wa Kijinsia, Migogoro ya Aridhi, Wivu wa Mapenzi, Ulevi, Ramli chonganishi na Tamaa.       

Katika Mkutano huo Komred Kheri James amewaomba na Kuwasihi viongozi wa Vijiji, Dini, Mila na Wananchi kwa Ujumla Kuheshimu na Kuhimizana Umuhimu wa Upendo, Utii wa Sheria na Kuzingatia Mafundisho ya Dini kama Nyenzo Muhimu ya Kupunguza na kumaliza Visasi, Chuki, Tamaa na Ukatili Miongoni Mwa Jamii.                                        

Akitoa Salamu za Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wilaya ya Mbulu, amewasisitiza Wananchi Kuacha Mara Moja Tabia ya Kujichukulia hatua Mikononi na amewaahidi Ushirikiano wa Kutosha ili kwa Kushirikiana na Jamii Uhalifu Uendelee Kudhibitiwa.                             

Mkutano huo Maalumu, Umehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mbulu Mji, Viongozi wa Vyama, Dini, Watumishi na Wananchi wa Kata ya Murray, ambao kwa Pamoja Wameazimia Kusimamia na Kudhibiti kila Sababu inayoweza Kusababisha Mauaji katika Eneo Lao.  

      

Share To:

Post A Comment: