Na Mwandishi Wetu,ARUSHA


WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Prof.Joyce Ndalichako,amesema hadi sasa vyuo vya ufundi na ufundi stadi,vimeanza kutekeleza agizo la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,alipoagiza  sekta ya elimu kujikita zaidi katika ukuzaji wa ujuzi kwa wanafumzi.

Aprili 22 mwaka huu,Rais Samia,akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,aliagiza sekta ya elimu kuwa anataka kuona kuwa elimu inajikita zaidi katika ukuzaji wa ujuzi.

Waziri Ndalichako,aliyasema hayo jana jijini Arusha,alipotembelea mabanda wakati wa maonyesho yaliyoandaliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi (NACTVET), yanayofanyika kwa siku tatu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Tumeshuhudia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,ilifanya kongamano kubwa la kuonyesha kazi ambazo walizofanya kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,alilotoa Aprili 22wakati akilihutubia Bunge.

“Katika sekta ya elimu aligiza kuwa anataka kuona kuwa elimu inajikita zaidi katika ukuzaji wa ujuzi kwahiyo katika maonyesho haya tunaona uhalisia wa kile ambacho Rais Samia aliagiza kwa kuwa vyuo vimeaza kutekeleza na kuimarisha mafunzo yao.aliongeza”

Pia alisema amejiridhisha kwamba kwa sasa vyuo hivyo,vinajitahidi kuwafundisha wanafunzi njia za kutatua changamoto katika jamii na mazingira yao.

“Katika sekta ya elimu aligiza kuwa anataka kuona kuwa elimu inajikita zaidi katika ukuzaji wa ujuzi kwahiyo katika maonyesho haya tunaona uhalisia wa kile ambacho Rais Samia aliagiza kwa kuwa vyuo vimeaza kutekeleza na kuimarisha mafunzo yao.aliongeza”

 “Tumeshuhudia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,ilifanya kongamano kubwa la kuonyesha kazi ambazo walizofanya kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,alilotoa Aprili 22wakati akilihutubia Bunge.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi,alisema maonyesho hayo yafanyika sasa kwa mara ya tano na wamekuwa wakivikutanisha vyuo hivyo na wadau ili kuwaonyesha Watanzania shughuli wanazofanya ikiwamo teknolojia wanazogundua na mafunzo yanayotolewa.

Kadhalika alisema kwenye maonyesho yatakuwa na washiriki 160 ambao wana vibanda lakini kwenye kongamano wako washiriki zaidi ya 300.

Pascal Marusu,Mkuu wa Idara Famasia,kutoka Chuo cha Sayansi za Afya cha KOLANDOTO,ambaye ni miongoni mwa washiriki katika maonyesho hayo,alisema kwenye maonyesho watapata fursa ya kuonyesha teknolojia na mafunzo kwa vitendo wanavyowafundisha wanafunzi kwenye chuo hicho.

Mkuu huyo wa Idara ya Famasia,akizungumza kwa niaba ya mkuu wa chuo,alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya afya kwa ngazi ya kati kwa kipindi cha miaka zaidi ya 60.

Alisema mambo wanayoonyesha ni kazi zinazofanyika katika chuo hicho,hasa kupima vipimo mbalimbali ikiwamo vya presha ya damu,uzito,sukari,kiwango cha sukari na kutoa ushauri.

“Pia  katika kitengo cha sayansi za ufamasia kuna baadhi ya bidhaa zimetengenezwa ambazo ni chache kadri ya nyingi tulizonazo ili kuwafundisha wanafunzi namna watengeneze wenyewe kwa ajili ya kuwatibu binadamu na wauguzi wanaonyesha jinsi wanavyowafanya kazi zao hasa wanapoawafundisha wanafunzi,”alisema.

Vilevile alisema wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo na wanapohitimu mafunzo wengi wao wanaajiriwa pia wako wengine wanajiajiri na kujiendeleza kulingana na malengo yake.

Share To:

Post A Comment: