Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

TAZAMA HII VIDEO

Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imekemea suala la wanaume kutelekeza familia zao na kwamba linasababisha mmomonyoko wa maadili pamoja na ukatili kwa watoto katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesungumzwa katika ziara ya kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakati ikitembelea miradi ya maendeleo na kukagua  uhai wa jumuiya kata ya Kizumbi na kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko pamoja na mambo mengine amekemea suala hilo huku akitaja athari zake ambapo pia ameiomba serikali kuchukua hatua kwa mzazi anayebainika kutelekeza familia na kwamba hali hiyo itasaidia kuimarisha familia.

“Baba anapomtelekeza mke na watoto, watoto wale nani atawatunza jambo hili kama wazazi tunalikemea mchezo huu wa Baba kutelekeza familia siyo jambo nzuri tunatakiwa tuwe na msaada mkubwa kwa wanaotendewa unyanyasaji huu, huyo Baba anatakiwa atafutwe akamatwe arudishwe mpaka nyumbani kwake lakini serikali inatakiwa kumchukulia hatua za kisheria”.

“Athari ya kwanza wanawake wengi wanakosa uwezo wa kuwasomesha watoto baada ya kuathirika kiuchumi utakuta watoto hawasomo hata kama watasoma lakini mavazi wanayovaa mara nyingi siyo ya heshima lakini ukweli ni kwamba suala hili ninawaathiri sana watoto na kusamabisha watoto kwenda mitaani kwa sababu wanakosa malezi bora ya wazazi wawili Baba na Mama”.amesema mwenyekiti Mrindoko

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi naye amekemea tabia za wanaume kukataa mimba baada ya kumbebesha ujauzito mwanamke ambapo amesema hali hiyo inawaathiri kisaikolojia wanawake na kupelekea ugumu wa maisha yao ya kila siku.

“Wapo baadhi ya wanaume wanatabia za kuwapa mimba wanawake halafu wanazikataa, mwanamke anabeba mimba miezi 9 mpaka anazaa akizaa analea huyo mtoto mpaka anakua mtoto akipata mafanikio Baba anajitokeza ndiyo maana unakuta watoto wengine siku hizi wanawakana wazazi, wewe unasifa gani ya kuwa Baba wakati ulimpa mimba mwanamke ukamkataa jiulize hivi angeitoa hiyo mimba ungejitokeza”.

“Niwaomba wanawake msikate tamaa mwanaume akikataa mimba wewe toa taarifa kwa viongozi husika halafu endelea kuilinda ukijifungua mlee mtoto bila malalamiko Mungu atakusaidia”. Amesema katibu wazazi Bi. Doris Kibabi

Baadhi ya wazazi nao wamekemea suala hilo huku wakiipongeza kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kufanya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika masuala mbalimbali ikiwemo ukatili, utunzaji wa mazingira pamoja na uimarishaji wa jumuiya hiyo.

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imeendelea na ziara kutembelea miradi mbalimbali ya maendelo pamoja na kukagua uhai wa jumuiya za wazazi kwenye kata ambapo leo Jumanne Mei 16,2023 imetembelea kata ya Kizumbi na kata ya Ibinzamata.

Wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo wametoa elimu katika masuala mbalimbali ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili, kuimarisha malezi ya watoto kwenye familia,  elimu na haki za watoto na afya huku wakisisitiza ushirikiano ili kuimarisha jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

 

 

Kamati ya utekelezaji CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Mei 16,2023 ikiendelea na ziara kwenda kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Bugayambelele kata ya Kisumbi Manispaa ya Shinyanga.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: