Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 19 Mei 2023 wameitembelea familia ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na familia hiyo ikiongozwa na mjane wa Hayati Sokoine Bi. Napono Sokoine ambao wamemshukuru kwa kuwatembelea kijijini hapo na kuipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha Makamu wa Rais na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wameweka shada la maua na kuongoza sala ya kumuombea Hayati Edward Moringe Sokoine katika kaburi lake lililopo katika eneo la nyumba hiyo.


Share To:

Post A Comment: