Bertha Mollel Arusha. Serikali imeamua kuunganishia Jeshi la polisi mifumo yote ya mawasiliano ya kiusalama kimtandao katika maeneo ya uhifadhi kwa ajili ya kupata taarifa za malalamiko kutoka maeneo mbali mbali duniani yanayahusu Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa mali asili na utalii Mohamed Mchengerwa katika hafla ya makabidhiano ya pikipiki 15 zilizotolewa na benki ya CRDB kwa jeshi la polisi kitengo cha utalii na diplomasia cha mkoani Arusha.

Alisema kuwa Serikali kupitia taasisi zake za utalii imefunga mifumo ya kisasa ya ufuatiliaji kupitia satelaiti ili kupata taarifa zote za uhalifu katika maeneo ya hifadhi na zile zinazoingizwa kwenye mitandao na watalii wetu wawapo nje ya hifadhi.

"Katika maeneo yote ya uhifadhi, tunazo taarifa nyingi sana za wahalifu kwa sababu ya mifumo ya kisasa tuliyoifunga ya ufuatiliaji kupitia satelaiti na vyanzo vingine lakini kupitia bodi ya utalii tunacho chombo kinachotusaidia kupata malalamiko yote ambayo nimeagiza wenzangu wahakikishe kinaanza kufanya kazi kuanzia sasa na polisi nanyi tunakwenda kuwaunga huko"

Alisema lengo la mifumo hiyo ni ili kupata malalamiko yote duniani yanayohusu Tanzania katika sekta ya utalii na kuchukua hatua za ufuatiliaji haraka iwezekanavyo na kuchukia hatua kabla haijaleta madhara katika harakati zetu za kukuza sekta hii muhim.

"Nakwenda kufanyia kazi kuhakikisha mifumo yote ya mawasiliano ya kiusalama kupitia bodi ya utalii , ngorongoro Tanapa, imeunganishwa pamoja na kituo cha polisi cha utalii ili na ninyi muwe na taarifa za kiusalama za kwenye maeneo yetu ya hifadhi lakini pia taarifa za kiusalama duniani zinazohusu Tanzania"

Mcherengwa alitumia nafasi hiyo kuipongeza benki ya CRDB kwa kutoa msada huo wa piki piki zitakazosaidia Askari kutekeleza majukum yao kiurahisi ikiwemo kufanya doria ili kuwasaidia kuimarisha usalama wa watalii.

Akitoa piki piki hizo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema wanayo furaha kubwa kukabidhi pikipiki hizo ili kuwasaidia askari kukimbizana na wahalifu wanaowapora watalii au kusafirisha mihadarati hivyo kuharibu sifa njema za jiji hili la kitalii.

"Tunaamini matumizi sahihi ya pikipiki hizi yatasaidia kudhibiti uhalifu jijini hapa na tunaahidi tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kupunguza baadhi ya changamoto zinazokwamisha ufanisi wake ili nchi yetu iendelee kuwa salama kwa biashara na uwekezaji,” amesema Nsekela.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Edith Swebe, amesema jitihada zinazoendelea kuutanga utalii wa Tanzania umelifanya Jiji la Arusha kupokea wageni wengi wanaoongeza haja ya askari polisi kuwapo katika kila eneo.

"Kwa sasa tunasimamia mradi wa utalii salama ambao unahitaji askari kuwapo kila walipo wageni, tunashukuru pikipiki hizi zitasaidia kuwafikisha askari kwenye maeneo ambako magari hayawezi kufika kwa urahisi zikiwamo barabara nyembamba"

Alitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali na wadau wengine wa utalii kuliwezesha jeshi hilo kupata pikipiki nyingine 10 zitakazofanya kata zote 25 za Jiji la Arusha kuwa na pikipiki moja ya doria kurahisisha utekelezaji wa mradi wa utalii salama.

Share To:

Post A Comment: