Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 


Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Dkt. Suleman Jafo ametoa maagizo kufuatia baadhi ya wananchi na Wafanyabiashara kubadilisha matumuzi ya vifungashio kuwa vibebeo na kutumia baadhi ya mifuko ya plastiki yaani vibebeo visivyokidhi matakwa ya kikanuni.


Amesema ni makosa kisheria kubadili matumizi ya vifungashio vigodo kuwa mifuko ya kibebeo ya bidhaa kwa mujibu wa sheria adhabu stahiki zitatolewa kwa watakao kiuka Sheria wakiwemo watengenezaji, wasambazaji na watumiaji wa vifungashio vya plastiki vinavyozalishwa au kuingizwa nchini na kutumika kama vibebeo.


Dkt.Jafo ametoa hayo leo Aprili 6,2023 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ambapo ametoa maelekezo kwa sekretariet za mikoa, Majiji Manispaa na halmashauri za wilaya zote nchini kuendelea kudhibiti matumizi ya vifungashio visivyo ruhusiwa kisheria kwa kuzingatia kuwa utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ni jukumu la wadau wote.


Waziri Jaffo amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa kupitia Ofisi zote za kanda za NEMC kuendesha Kampeni za kuondosha mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku.




Tarehe 26 Agosti, 2022, nikiwa kama Waziri mwenye dhamana ya mazingira nilitoa taarifa kwa umma kuendelea kusisitiza marufuku ya matumizi ya vifungashio kutumika kama vibebeo hususan kwa bidhaa za masokoni, Hali hii inaonesha ukiukwaji mkubwa wa Kanuni ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki unaofanywa na baadhi ya wazalishaji na wasambazaji ambao wamebadilisha mifuko laini ya plastiki isiyokuwa na mishikio na kuitumia kama vibebeo vya bidhaa. amesisitiza Dkt.Jafo


Aidha Waziri huyo ametoa kipindi cha siku thelathini (30) kwa meneja wa NEMC Mikoa kusimamia sheria na vifungashio hivyo visionekane ndani ya Hizo siku ambapo ni kipindi cha mwezi mmoja.


Nendeni mkasimamie katika maeneo yote meneja wa kanda atakayeshindwa kusimamia na Kuondoa tabia hiyo katika kanda husika atakua ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi. Amesema Dkt



Ikumbukwe kuwa tarehe 1 Juni, 2019, Serikali ilipiga Marufuku Uzalishaji; Uingizaji nchini, Usafirishaji nje ya nchi; Usambazaji; na Matumizi ya mifuko ya plastiki. Mafanikio ya marufuku hii yamewezesha kuimarika kwa hali ya usafi wa mazingira hususan maeneo ya mijini sambamba na kuongezeka kwa matumizi ya mifuko mbadala ikiwemo non-woven na mifuko ya karatasi; na fursa za ajira kwa wazalishaji wa mifuko mbadala.






Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: