Wananchi wa tarafa ya  Mbuguni  wilaya ya Meru   mkoani Arusha  Wametoa kero zao  mbalimbali  zinazo wakabiri katika maeneo yao wanayoishi ikiwemo maji  ya nayo toka katika  Mito mbalimbali  kujaa mashambani mwao  na kusababisha  mazao yao kufa. 

Kero hizo wamezitoa katika ziara  inayoendelea kufanyika na Umoja wa wanawake  Tanzania  kupia chama cha Mapinduzi UWT  wakiongozwa na mwenyekiti  wa UWT  Wilaya ya Meru  Juliet  lameki Maturu huku Mgeni Rasmi akiwa mwenyekiti wa UWT Mkoa  Flora Zelothe. 

Mvua zinazoendelea  kunyesha na kusababisha Mito ili pembezoni na tarafa hiyo  kufurika maji   yanayokqenda mojakwa moja kwenye mashamba na makazi ya watu imekuwa changamoto  kubwa kwa Wakazi wa eneo hilo  na hivyo wameiomba serikali  iwasaidie  kutengeneza muelekeo wa maji

Pia wamekuwa na changamoto ya kukosa maji safi na salama  nakupelekea magonjwa   ya tumbo kwa watoto na watu wazima vile vile  wamehamasisha upandaji miti katika maeneo yao hususani eneo la shule ambapo viongozi  wametembelea. 


Huku Diwani wa  kata ya Majengo  Bernad Wilson kivondo  akiuomba uongozi  wa UWT  kulifanyia kazi suala ilo kutokana na kuwa kero kubwa kwa wananchi wake. 

" nimejitahidi sana kufuatilia suala hili kwa kina ili kiweza kuondoa maji haya na nilimcuata mpaka muheshimiwa Mbunge ili aweze kutatua hii changamoto alihaifi kuja leo lakini majukumu mengine yamembana hivyo  naom a uongozi wa UWT  mtusaidie katika hili " amesema Diwani Kivondo. 

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Zelothe  amehaidi kuzifsnyia kazi changamoto  hizo huku akiwataka wekinamama kupendana  na kuto kukatishana tamaa ili waweze kukua kiuchumi na kuwa viongozi bora kuanzia kwenye familia zao. 

"Wanawake hatupendani  kabisa ukimuona mwenzio anagombea viongozi unaanza kumkatisha Tamara kumsema kuwa ataweza kufuingoza yile na akiwa kiongozi waanza kumsema tumemchagua ameanza kuringa hii inatukisesha kukua hasa katika uchumi" 

Pia amewataka  wanawake ambao hawajapata mkopo wajiunge na vikundi vilivyosajiliwa ili waweze kupata mkopo  huku akisisistiza wale waliopata mkopo na hawajarudisha warudishe mara moja ili wengine waweze kupata. 

Ametoa rai  kwa madiwani wa tarafa hiyo  kuita vikao na kueleza mapato na matumizi yalitotumika katika tarafa hiyo mara kwa mara  ili kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu mambo yanayotendeka na serikali  ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan


Share To:

Post A Comment: