Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mazishi ya mfanyabiashara wa nafaka Bwana Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food yamefanyika leo Alhamis April 6,2023 Nyumbani kwake kata ya Kambarage mjini Shinyanga.

Bwana Boniphace Makilagi aliyefariki Dunia wiki hii siku ya Jumatatu April 3, 2023 akiwa Jijini Mwanza.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi wa serikali, viongozi wa Dini, vyama na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga na nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Mazishi ya marehemu Bwana Boniphace Said Makilagi yamefanyika  nyumbani kwake ambapo misa ya mazishi imeongozwa na Padre Benedick Magaba wa kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Gasper jimbo kuu la Dar Es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba huo amesema serikali itaendelea kushirikiana na familia ya marehemu Boniphace Makilagi huku akiwasihi kuendelea kuyaishi meya aliyoyaacha katika maisha yao ya kila siku.

Aidha baadhi ya viongozi wa serikali na chama kutoka sehemu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Samizi wameeleza namna walivyoguswa na msiba wa Boniphace Makilagi jina maarufu Musoma Food huku wakitoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Bwana Boniphace Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na amekuwa akipata matibabu nchini Kenya na India.

Alipata nafuu  ambapo  kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa, mnamo tarehe 3.4.2023 aliugua ghafla jijini Mwanza na kufariki dunia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Boniphace Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha mjane na watoto wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga. 

Viongozi wa serikali, Dini na viongozi  mbalimbali wa vyama vya kisiasa wakiwa  kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga

Share To:

Misalaba

Post A Comment: