Na Magesa Magesa,Arusha


WALIMU wametakiwa kuhakikisha kuwa wanakopa kwenye taasisi za kifedha
zilizopo kwa mujibu wa sheria na kuacha kukopa katika taasisi umiza za
kifedha ambazo nyingi ni za kitapeli na  zimekuwa zikitoza riba kubwa
pamoja na kuwatapeli.

Ofisa ushirika wa jiji la Arusha, Omary Mrugeni aliyasema hayo jana
alipokuwa akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wanachama wa Chama cha
kuweka na kukopa (SACCOS)cha waalimu wa jiji la Arusha

Amewataka waalimu kuhakikisha kuwa wanakopa katika vyama vyao ili
kuimarisha ushirika na kuviongezea ji uwezo  ambapo pia amewataka
viongozi pamoja na watendaji kuhakikisha kuwa wanaendesha vyama vyao
kwa kufuata taratibu kanuni na misingi ya ushirika.

Awali Mwenyekiti wa Chama hicho cha kuweka na kukopa cha waalimu wa
jiji la Arusha(Arusha Teachers SACCOS)Mwl.Ahamonhery Zelote alisema
kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu kwa wanachama ili waweze
kujua umuhimu wa ushirika,wajibu na haki zake katika chama.

Alitoa wito kwa waalimu wengi zaidi kujiunga na SACOOS hiyo na kueleza
kusikitishwa kwake kwani jiji la Arusha lina zaidi ya waalimu 2000
huku wanachama wakiwa ni 472 ambapo amewataka wanachama kuwahiza
waalimu wenzao kujiunga nao.

“Changamoto kubwa tunayokutana nayo ni uelewa mdogo juu ya ushirika
kwa wanachama na ndio maana tumeandaa warsha hii,nipende kuwataka
wanachama kuhakikisha kuwa mnazingatia elimu mtakayoipata na kuifanyia
kazi kwa vitendo”alisema Zelote.

Kwa upande wake Meneja wa chama hicho,Edna Laizer alieleza kushangazwa
na baadhi ya wanachama wao kukimbilia kukopa katika mabenki na taasisi
mbalimbali za kifedha ambapo wamekuwa wakitumia muda mrefu kufuatilia
mkopo pamoja na kutozwa riba kubwa.

Meneja huyo amemtaka kila mwanachama  wa  chama hicho kuhakikisha kuwa
anazingatia haki na wajibu wake katika chama kwani kwa kufanya hivyo
atakuwa na uwezo wa kujenga na kukuza mtaji wa chama.

Katika warsha hiyo mada mbili ziliwasilishwa ambazo ni haki na wajibu
wa mwanachama pamoja na kujenga na kukuza mtaji wa chama ambapo baadhi
ya washiriki Mwl Abdul Mmbaga na Samwel Mkhandi walipongeza kupatiwa
mafunzo hayo na kueleza kuwa yamekuja muda muafaka.

“napongeza kwa kupatiwa mafunzo haya na nitakuwa balozi mzuri kwa
wengine na nakipongeza chama kwani kimekuwa kikitupatia mkopo kwa muda
mfupi na riba nafuu pamoja na kupata gawio kutokana na faida
inayopatikana”alisema mwl.Mkhandi.
Share To:

Post A Comment: