Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mashirika mawili yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo learing kwa kushirikiana na serikali yamekutana na watendaji  mbalimbali ngazi ya kata na Mitaa kwa lengo la kujadili namna bora ya kutatua changamoto ya watoto wanaoishi mitaani.

Kikao hicho kimefanyika leo April 18, 2023 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na  kuhudhuriwa na maafisa watendaji wa kata, wenyeviti wa serikali za mitaa, pamoja na maafisa wa jeshi la polisi ngazi ya kata katika Manispaa ya shinyanga

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Ezra Manjerenga pamoja na mambo mengine ameeleza malengo ya kikao hicho kuwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kuwaondoa  watoto kuishi kwenye mazingira hatarishi.

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo pamoja na maelekezo mbalimbali amewataka wenyeviti wa mitaa  kushirikiana ili kuwabaini watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

“Majukumu yenu ni kuhakikisha mnawafahamu watoto na kuzibaini Familia zao, mnatakiwa kuwa na takwimu sahihi za watoto wenye changamoto hiyo, mnatakiwa kusaidizana na maafisa ustawi wa jamii pamoja na viongozi na wadau wengine katika kutatua tatizo hili lakini mnatakiwa kuwa na mipango yenu ya kumaliza tatizo la watoto wa mtaani na mnatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za juu pale mnapokutana na changamoto lakini pia kutoa taarifa kwa wadau wa shirika hili, mnatakiwa kufanya uhamasishaji kwenye jamii hasa mnapokuwa na mikutano yenu ya hadhara suala la malezi bora kwa watoto liwe ni kipaumbele ili wazazi wajue hali halisi ya changamoto hii lakini pia mnatakiwa kuweka makubaliano ya pamoja na wazazi juu ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kuzingatia umri wa watoto kuajiriwa”.Amesema Afisa ustawi wa jamii Elizabeth Mweyo

Nao baadhi ya wenyeviti wa mitaa kutoka kwenye kata mbalimbali ikiwemo kata ya Ndala, Kitangili, Chamaguha pamoja na kata ya mjini wamelipongeza shirika la Nancy Foundation kwa ubunifu huo huku wakiahidi kutoa ushirikiano kwa serikali pamoja na mashirika hayo katika utekelezaji wa mradi huo.

Mashirika hayo mawili Nancy Foundation na Ubongo learing yanatekeleza mradi wa Miezi mitatu unaolenga kupunguza au kumaliza kabisa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza leo April 18,2023 katika kikao cha pamoja na watendaji mbalimbali ngazi ya kata ya mitaa Manispaa ya Shinyanga

Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza leo April 18,2023 katika kikao cha pamoja na watendaji mbalimbali ngazi ya kata ya mitaa Manispaa ya Shinyanga

Afisa ustawi wa jamii Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leopald Hamza akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023.

Mtendaji wa kata ya Ndala Bwana Joshua Masengwa akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Polisi wa kata ya Ndala Bwana Alimpa Willa akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mitimirefu kata ya Mjini Shinyanga Bwana Nassor Mokh Warioba akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa mtaa wa Banduka Bwana Pius Mathias akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mtendaji talafa ya Shinyanga mjini Bwana Mathias Masalu akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akiwa katika kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ancila Katero akiwa katika kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Watendaji wakiwa katika kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Polisi wa kata ya Kitangili Alinsp Shaweji Halahala wa kwanza upande wa kulia, polisi wa kata ya Mjini Shinyanga Alinsp Jane Mwazembe katikati pamoja na polisi wa kata ya Ndala Alinsp Alikwin Willa kutoka upande wa kulia wakiwa kwenye kikao leo April 18,2023.

Mratibu wa usambazaji kutoka Ubongo learning upande wa kulia akiwa katika mazungumza na Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Lemiflora Nyalaja kwenye kikao leo April 18,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: