Na Farida Mangube, Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali inaendelea kuhakikisha maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Waziri Prof.Ndalichako amesema Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa sheria namba tano ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

Waziri Prof.Ndalichako alisema hayo mkoani Morogoro kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pakazi ambapo alisema Serikali inaendelea kuhakikisha maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Aidha alisema kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (Osha) Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi nchini sambamba na kuwataka waajiri wa sekta za umma na binafsi kuzingatia usalama mahala pa KAZI kwa wafanyakazi wao.

Alisema Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Sheria namba tano ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 miongoni mwa wadau na Watanzania wote kwa ujumla.

“Lengo ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi,”aliesema

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (Osha), Hadija Mwenda amesema watahakikisha mazingira ya ufanyaji kazi nchini yanakuwa salama huku akiwataka wafanyakazi kujiunga na wakala huo.

"Nikuhakikishie Mheshimiwa Mgeni rasmi, OSHA kwa kushirikiana na wadau imekua mstari wa mbele kuwahimiza Waajiri kuzingatia na kutekeleza Matakwa ya Sheria ya kazi 2003." Alisema.

Aidha aliwataka wafanyakazi kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa mahala pa Kazi ili kuepesha migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Meneja usalama, afya, mazingira na ubora wa Cherry Garments and Safety Solutions Rose Lembrice alisema wao kama wadau was OSHA wameshiriki Katika maonyesho hao ili Kutoa Elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuzingatia usalama na afya mahali pakazi

Alisema Katika kuzingatia usalama na afya mahali pakazi ni lazima wafanyakazi wawe na vitendea kazi vyenye ubora na vilivyothibishwa na mamlaka husika.

Akitoa Salama za waajiri mfisa mtendaji Mkuu ATE Suzanne Ndomba alisema ni vyema kwa waajiri nchini kuweka mazingira salama kwa wafanyakazi wao katika maeneo ya kazi kama ambavyo kanuni na sheria mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa zimekua zikielekeza.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa Mwaka Huu inasema “Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi” (A safe and healthy Working Environment is a Fundamental Principle and Right at Work)”.

Share To:

Post A Comment: