Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga amehoji siku ambayo vituo vya afya vitasajiliwa kwenye Bima ya Afya ili wananchi waanze kuhudumia.


Na Fredy Mgunda, Dodoma.

MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga amehoji siku ambayo vituo vya afya vitasajiliwa kwenye Bima ya Afya ili wananchi waanze kuhudumia.


Akiuliza swali la nyongeza Bungeni Mjini Dodoma Jana Aprili 13, 2023 Mbunge Nyamoga ametaja vituo hivyo kuwa ni Ng’uruhe, Ruahambuyuni, Ilula pamoja na Nyalumbu.


Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amemshauri Nyamoga kupeleka orodha ya vituo vya Afya ambavyo havijasajiliwa viangaliwe kama vina vigezo.


Amesema ikiwa vituo hivyo vitakidhi vigezo vitasajiliwa na vitatoa huduma.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: