Na, Imma Msumba ; Wanging'ombe

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 umeendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Wangingombe Mkoani Njombe kwa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kituo cha afya cha Usuka ambapo kituo hicho kilipokea fedha za tozo shilingi milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa Kituo hicho.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe hilo la msingi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdallah Shaibu Kaim amepongeza ujenzi wa Kituo hicho na kuwataka wasimamizi wa ujenzi wa Kituo hicho kuongeza umakini wakati wa kushuhulikia kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho.

"Niwasisitize wasimamizi wa miradi na wahandisi kuzingatia wakati wa kukamilisha miradi kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi hii mkafanye kazi kwa bidii usiku na mchana ili watanzania na walengwa wa miradi wakanufaike kama ambavyo serikali imetarajia" Alisema Kiongozi

Kwa upande wake Mkazi wa kijiji chaUsuka Leah Samwel ,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha za kujenga kituo cha afya Usuka kwani kituo hicho kitawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya na kuacha kufanya shughuli za maendeleo ambazo zinawawezesha kuwaingizia kipato.

"Kwakweli niwapongeze sana  viongozi wa ngazi ya Wilaya na Mkoa kwa ushauri na usimamizi wao uliopelekea ujenzi wa kituo hichi kukamilika kwa wakati maana tulikuwa tunatembea umbali mrefu sana kutafuta huduma za afya,kwani kukamilika kwa kituo hiki kitatusaidia sana sisi wananchi wa Kata hii ya Usuka " Alisema Leah

Share To:

Post A Comment: