Na John Walter-Manyara

Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM kitaifa inatarajia kufanyika Kijiji cha Galapo wilaya ya Babati mkoani Manyara huku mada za maadili na malezi zikitawala zaidi.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Mei 3, 2023 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Mkoa wa Manyara  Johanes Darabe  alipokuwa akizungumza na Smile fm redio kuhusu maandalizi ya wiki hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema kutokana na kuwa kwa  mmomonyoko wa maadili katika jamii,  jumuiya hiyo imeamua kuvunja ukimya na kujadili juu ya  changamoto hiyo na utatuzi wake.
Amesema uzinduzi wa wiki ya Wazazi utafanyika katika uwanja wa Galapo  Mei 6,2023 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa Dogo Iddi Mabrouk.
Amesema tayari maandalizi yanafanywa na viongozi katika wilaya zote za mkoa wa Manyara kuelekea siku hiyo itakayohitimishwa Mei 9.
Darabe amesema watatembelea taasisi za Jumuiya, Shule mbalimbali kutoa elimu kuhusu maadili na shughuli nyingine za kijamii.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi wote, wananchama wote wa chama cha mapinduzi na jumuiya zote za chama cha mapinduzi kushiriki kwenye uzinduzi wa maadhimishi hayo.
Kauli mbiu ya wiki ya Wazazi mwaka 2023 "Taifa bora hutokana na malezi bora ya watoto"
Share To:

Post A Comment: