Na, Imma Msumba : Ludewa 

Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Njombe Ukitokea Mkoani Ruvuma ulipomaliza shughuli zake ambapo utakimbizwa katika Wilaya Nne zenye Halmashauri Sita za mkoa wa Njombe huku miradi yenye thamani zaidi ya shillingi billioni tisa nukta tatu ikitarajiwa kukaguliwa kuwekewa mawe ya msingi Pamoja na kuzinduliwa.

Akizungumza katika Makabidhiano hayo Katibu Tawaia wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary Ameeleza kuwa Kauli mbinu ya Mwenge wa Uhuru 2023 imezingatia umuhimu wa mabadiliko ya Tabia nchi katika uhifadhi wa mazingira sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Hata hivyo amesema kwamba wao kama Mkoa wa Njombe wamefanikiwa na kuendeleza mikakati ya utunzaji wa mazingira husasani upandaji wa miti ambapo mkoa huo umevuka lengo la kupanda miti Zaidi ya Milioni Hamsini kuanzia mwaka 2022 hadi kufikia mwaka huu ambapo tofauti ya lengo lililowekwa la kupanda miti milioni tisa kwa mwaka mmoja.

“Mkoa wetu unazaidi ya vyanzo elfu tatu vya maji ambavyo tunaendelea kuvitunza na kuvihifadhi kwa kuendelea kupanda miti ambayo ni rafiki na mazingira” Alisema Judica 

“Tumeendelea kuhamasisha falsafa ya mwenge wa uhuru katika kudumisha upendo,utulivu, umoja na mshikamamo wa taifa letu pia mkoa Njombe tumeendelea kuhamasisha jamii dhidi ya mapambano ya rushwa,dhidi ya ukimwi na dawa za kulevya na suala nzima la lishe bora katika jamii yetu” Aliongezea

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimeanza kwa kukimbizwa katika Wilaya ya Ludewa ambapo umekimbizwa katika Kilomita 173 ndani ya Vijiji nane ambapo umeweka mawe ya msingi katika Vyumba wiwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Ngelenge,kukagua shamba la korosho la mwananchi,Kuzindua nyumba ya kulala wageni,kufungua Zahanati ya Kimelembe,kuzindua klabu ya wapinga Rushwa,na kukagua hifadhi ya mazingira na vyanzo vya maji,kukagua maendeleo ya ujenzi ya Jengo la Utawala la Halmashauri, miradi yote yenye thamani ya bilioni mbili milioni mia mbili arobaini na mbili.

Hata hivyo Kiongozi wa Mbio za mwenge Abdallah Shaibu Kaim ameonyesha kutoridhishwa kwa kusasua kwa ujenzi wa jingo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambapo ameagzia wasimamizi kuhakikisha ujenzi wa jingo hilo unakamilika kwa wakati unatakiwa, huku akisistiza ujenzi huo uendane sambamba na thamani ya fedha.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amekiri kupokea maelekezo kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote kama yalivyotolewa.

 Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amemshukuru jitihada zinazoendelea kufanya na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea wananchi wa ludewa maendeleo mbalimbali ikiwemo huduma ya Afya katika Zahanati ya Kimelembe ambapo alipiga goti mbele ya wakimbiza mbio za mwenge kitaifa kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa Zahanati hiyo.

 

Share To:

Post A Comment: