Na;Elizabeth Paulo,Dodoma


Kufuatia bajeti ya shilingi billioni 954 ya mwaka wa fedha 2022/23 ya Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wametia saini Miradi minne (4) ya Umwagiliaji Yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 41.


Katika bajeti hiyo ya shilingi bilioni 954 wabunge waliidhinisha zaidi ya shilingi billioni 361 Kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo nchini hasa katika changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi.


Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji Wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa alipokua akizungumza katika hafla ya utuaji saini kwa Miradi hiyo iliyofanyika katika ofisi za wizara ya kilimo jijini Dodoma.


Mndolwa amesema miradi hiyo inatekelezwa katika mikoa ya Tanga Jimbo la Korogwe mji, Mara Jimbo la Rorya, Singida Jimbo la Iramba Mashariki na Tabora huku watekelezaji wakiwa ni wakandarasi Wazawa kwa asilimia 80%.


“Leo ni katika muendelezo wa kazi ambazo zilikabidhiwa kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji za kuleta tija ya kilimo kwa wananchi”


Nao baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Rorya Jafari Wambura amesema mradi huo ni Mradi mkubwa ambapo ukikamilika zaidi ya Mia Tisa mpaka elfu moja watanufaika na mradi huo ndani ya jimbo lake.


Kwa upande wake Francis Isack Mbunge wa Mkalama Amesema mradi huo ni mkubwa katika Jimbo lake na iwapo utakamilika kwa wakati wananchi watakua wamenufaika hivyo amemtaka mkandarasi kufanya kazi kwa kiwango na weledi.


Naye Mbunge wa Korogwe Mjini Dkt.Alfred James amesema wananchi wa Jimbo Hilo hususani Wakulima wa Mpunga wamekua na changamoto hivyo mradi huo wa Skim ya Mahenge itawasaidia na wamekua wenye furaha kupata mradi huo.








Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: