Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida wakifanya usafi wa mazingira katika maeneo ya ofisi yao ikiwa ni moja ya shughuli kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kilele chake kitakuwa kesho Aprili 26, 2023.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida, wamefanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya ofisi yao ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ambaye alizitaka taasisi zote za Serikali mkoani hapa kufanya shughuli za usafi wa mazingira ikiwa ni moja ya jambo muhimu kuadhimisha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kilele chake ni kesho Aprili 26, 2023.

Meneja wa NSSF) Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana wakati wa zoezi la kufanya usafi alisema wanafanya usafi huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa la kuzitaka taasisi zote za umma mkoani hapa kufanya hivyo.

Alisema kufanya usafi ni jambo jema kwani unayafanya mazingira ya ofisi kuwa mazuri na bora pia ni afya ambapo aliwataka watumishi wa NSSF mkoani hapa kuendelea kufanya usafi wakati wote.

Akizungumzia kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar alisema umetela amani na utulivu mkubwa katika pande zote mbili jambo ambapo limechangia mfuko huo kuwa na mafanikio makubwa ya kuweza kuwalipa wanachama wao kwa wakati na kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini likiwepo daraja na Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kalimilwa aliwataka wananchi wa pande zote mbili kuendelea kuwapongeza wahasisi wa muungano huo Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuanzisha muungao huo ambao umeleta tija kubwa na akatumia nafasi hiyo kuwashukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Dk.Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar kwa kuulinda muungano huo.

Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alizifuta sherehe za miaka 59 ya Muungano na badala yake alitaka sherehe hizo kwa mwaka huu zifanyike katika ngazi ya kimikoa kwa kufanya usafi wa mazingira na shughuli zingine za kijamii na kiuchumi badala ya kufanyika kwa gwaride kama ilivyozoeleka.

Meneja wa(NSSF) Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana wakati wa zoezi hilo la kufanya usafi.

Ufanyaji usafi ukiendelea.
Kazi ya usafi katika maeneo ya ofisi hizo ikiendelea.
Usafi ukiendelea.
Kazi ikiendelea.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: