Na Denis Chambi, Tanga.

MWENYEKITI wa chama cha  ACT  Wazalendo  Zitto Kabwe ametoa mapendekezo kwa vyama vyote vya  siasa hapa nchini kuunda tume ya kitaifa itakayohusika kusimamia  na kuangazia maswala  haki na ukweli   hii ikilenga kufanya uchunguzi na  kuondoa utengano wa kimaslahi kupitia nyanja mbalimbali kwa maslahi mapana watanzania.

Akizungumza mkoani Tanga katika mkutano wa hadhara na wanachama wa chama hicho march 8,  2023  Zitto alisema  kuwa licha ya michakato mingi ya kisiasa inayofanyika hapa nchini kila chama kikisimamia sera zake kuna haja ya kuunda tume mahususi kwajili ya kuangazia haki na ukweli itakayo kuwa na lengo la kutatua changamoto  mbalimbali za kisiasa  zilizojitokeza  na zitakazojitokeza kwa wananchi na viongozi wa  vyama vya siasa  ambapo wengi wanaweza kungia katika migogoro katika harakati za kutafuta haki zao.

"Tumekuwa tukisistiza kwamba kuna haja nchi yetu iwe na tume ya haki na ukweli  ili kila mtu ambaye aliumizwa kwa namna yeyote ile aweze kupata msaada  wakiwemo waliozushiwa kesi yeyote, waliofungwa kwa makosa mbalimali yakiwemo ya jinai na mengineyo  haya yote yanahitaji tuwe na  tume ya uchunguzi ambayo  iyayatazama mambo haya ili wale ambao walionewa  na kunyang'anywa mali zao,  makosa ya jinai wafutiwe makosa yao hapo ndipo tunaweza kusema nchi inapona hatuwezi kuiponya nchi hii kwa kufunika mambo" alisema Zitto.

Pamoja na hayo chama hicho cha ACT Wazalendo kimeitaka serikali  kuangalia upya suala la mswada wa Bima ya afya kwa wote ambao ulishindwa kupitishwa na  muhimili wa Bunge   kutokana na kutoridhishwa   nao ikiwemo gharama zinazotakiwa kuchangia ambapo bado kimeona kuwa itakuwa ni mzigo mzito kwa wananchi.

Alisema kuwa kupitishwa kwa mswada huo bado serikali itakuwa haijamsaidia mwananchi kutokana na gharama kuwa kubwa licha ya hali ya kipato chake kuwa chini ambapo kila mwananchi anapaswa kuchangia kiasi cha shilingi  laki tatu na elfu arobaini (340, 000)  kwa mwaka.

"Mswada ambao serikali imeupeleka ili kutunga sheria ya bima ya afya ni mswada ambao utaendelea kutukalisha watanzania kwa sababu  ni mswada ambao unaiondoa serikali kwenye jukumu lake la kushughulikia na kuhudumia  wananchi wake inapeleke mzigo ule kwenu wananchi na huku  serikali  haichangii chochote"  

"Wazo letu sisi tunataka serikali ichangie kwenye gharama za afya ambazo watanzania wanagharamia hatutaki ijitoe kwenye mfumo wa bima ya afya kama ambavyo serikali  inawachangia pensheni watumishi  wa umma ndio hivyo hivyo tunataka mwananchi ambaye anachangia kwenye bima ya afya ndio maana tunasema tunataka Taifa la wote maslahi ya wote" aliongeza Kiongozi huyo
 
Katibu mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu  ameipongeza serikali ya awamu ya 6  ya chama tawala chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini mara baada ya kufungiwa kwa mika kadhaa iliyopita hatua ambayo imeonekana kuleta matumaini mapya kwa watanzania kupitia vyama mbalimbali.

"Tangu uchaguzi mkuu umalizike mwaka 2020 sisi ACT Wazalendo  tulijitahidi kupambana kuhakikisha tunaongoza njia katika mageuzi ya  msingi ya kisiasa Tanzania,  kabla ya serkali ya awamu ya 6 kuingia madarakani sisi tulichukua hatua ya kukubali kushiriki mazungumzo ya kisiasa tuliona umuhimu wa maridhiano ya kitaifa  tunaamini usipoongoza utaongozwa, " alisema

Aidha  katibu huyo alisema kuwa harakati za chama hicho kupitia  mikuano walitoshiriki na vyama vya siasa ilivyofanyika hapa nchini  licha ya kuonekana matokeo chanya  na maridhiano bado  hakikusita kueleza umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya itakayoleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kiuchumi,  kibiashara   na kijamii huku akipendekeza kuwepo na mkutano wa kitaifa wa kikatiba utakaosaidia kupatikana kwa   katiba mpya.

"Tumeshiriki mazungumzo mbalimbali  yaliyoitishwa na baraza la vyama vya siasa Tanzania  , tumeshiriki pia mazungumzo yaliyoitishwa na  kituo cha demokrasia Tanzania kila mahala tulisema kwamba ili nchi hii ipone kisiasa kiuchumi na kijamii tunahitaji katiba  mpya na hatujaishia tu kwenye katiba mpya bali tumeeleza kuanzia marekebisho ya kisheria zinazoongoza mchakato wa katiba mpya "

Awali akizungumza makamu  Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania bara  Doroth Temu alisema bado suala la kukosekana kwa chakula cha kuyosha na kupanda kwa bei za vyakula hapa nchini imekuwa ni maumivu kwa wananchi wa hali za chini hali ambayo inaweza kuchangia wengi wao kushindwa kumudu gharama za vyakula akiiomba serikali kuendelea kutafuta suluhisho kwa mslahi mapana ya watanzania.

"Tunaingia msimu wa kilimo lakini bado bei za vyakula zipo juu sana,  kila tunapopita hilo limekuwa ni  kilio kwa wananchi wote,  Suala la njaa wasilifanyie dhihaka,  wananchi wa kipato cha chini wana maisha magumu  mno uwezo wa Taifa kulisha watu wake  kupata uhakika wa kupata chakula kwa bei  nzuri ni suala nzuri katika ujenzi wa Taifa serikali bado haijaja na majibu ambayo yanamsaidia mwananchi wa kawaida   kweli bei ya chakula imepanda na gharama zimekuwa maumivu" alisema Doroth.

" Sisi tumependekeza kwa serikali  kama suluhisho la muda mrefu tuhakikishe tunawawezesha wakulima kufanya kilimo cha kisasa kuwapatia pembejeo kwa bei nafuu ili hawa wakulima waweze kuzalisha chakula kingi zaidi lakini  tunafahamu serikali imetoa kibali cha kuagiza  tani elfu 90 za mchele  hivyo kama suluhisho la muda mfupi tunaitaka serikali ihakikishe kwamba chakula kinapofika nchini kinagawanywa na kusambazwa kimfikie mtu wa  kawaida kwa bei nafuu" alisistiza

Aliongeza kuwa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kila halmashauri ambazo o hutengwa  ili kuyawezesha makundi ya akina mama,  vijana na watu wenye ulemavu bado kuna malalamiko ya kuwepo kwa  mlolongo mrefu wengi wao wakishindwa kupata fedha hizo kwa wakati na hatimaye huhutana na na kushibwa kuchangia pato la Taifa.

" Wanawake wanalia mikopo  tumesikia sasa hivi kuna mikopo ya kausha damu ,  wanawake wanahitaji kuwezeshwa wapate mikopo yenye riba nafuu ,  hii mikopo wengi wamekuwa wakiihangaikia lakini hawaipati  kutokana na mchakato kuwa  mrefu ni wakati sasa wa kuhakikisha kwamba tunawapunguzia wanawake mateso ya kupata  mitaji ikiwemo  kila mwanamke angalauaweze kupata huu mkopo wa halmashauri usio kuwa na riba ili naye aweze  kuchangia katika pato la Taifa." alisema


Baadhi ya wanachma wa chama cha ACT Wazalendo wakifwatilia hotuba ya kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe katika mkutano wa hadhara uliofanyika March 8, 2023 kwenye uwanja wa Tangamano jijini Tanga.


Share To:

Post A Comment: