Wakala wa Vipimo Mkoani Geita imetoa siku 30 kwa Wauzaji na mawakala gesi  kuhakikisha wanakuwa na mizani ya kupimia Ujazo  stahiki wa gesi kama sheria inavyowataka kuwa na vipimo sahihi.

Wito huo umetolewa  mapema leo na Meneja wa  wakala wa  Vipimo Mkoa wa Geita , Balisco Kapesa  wakati akiongea na  mawakala pamoja na wafanyabiashara   Mkoani humo.

 

Amesema bado wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaouza mitungi ya gesi bila kupima kitu ambacho ni kinyume na sheria kwani uzito unatakiwa kuonekana kabla ya mtumiaji wa mwisho hajaanza kutumia.

 

“Ni kosa kisheria kuuza gesi bila kuwa na mizani kwahiyo mnapaswa kuhakikisha mnakuwa na mizani ili kuepuka hatua Kali za kisheria kwa wale watakaobainika  niombe ifikapo Aprili 1,2023 wote muwe na mizani”Balisco Kapesa Meneja wa wakala wa Vipimo Mkoa wa Geita.

 

Kapesa ameongezea kuwa ni vyema kwa  mtumiaji wa gesi akaona na  kuhakikisha  muuzaji akiwa amepima na amejiridhisha kabisa kuwa ni kiwango stahiki na kama ni pungufu  anaona.

“Niwaombe ndugu zangu Wafanyabiashara tushirikiane kutoa elimu Kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kupima gesi kabla ya kuchukua  kwani itawasaidia kujua ujazo na nyie kuepukana na lawama zisizokuwa za msingi ambazo nyingine zimekuwa zikipelekea kuchafua baadhi ya makampuni”Balisco Kapesa Meneja  Wakala wa Vipimo Geita.



Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: