Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akikabidhiwa Jarida la “Hazina Yetu” Toleo la Tano, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza kitengo hicho kwa uandaaji mzuri wenye ubunifu, ubora na kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na uelimishaji kwa umma katika masuala ya fedha na uchumi wa Taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya kukabidhiwa Jarida la “Hazina Yetu” Toleo la Tano, katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza kitengo hicho kwa uandaaji mzuri wenye ubunifu, ubora na kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na uelimishaji kwa umma katika masuala ya fedha na uchumi wa Taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akisoma Jarida la “Hazina Yetu” Toleo la Tano, baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (hayupo pichani), katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza kitengo hicho kwa uandaaji mzuri wenye ubunifu, ubora na kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na uelimishaji kwa umma katika masuala ya fedha na uchumi wa Taifa.

Katibu wa Waziri wa Fedha, Bw. Geoffrey Kesase na Katibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Fatma Shaaban, wakifurahia Jarida la “Hazina Yetu” Toleo la Tano, katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dar es Salaam)
Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amepongeza ubunifu na ubora wa Jarida la Hazina Yetu Toleo la Tano ambalo limeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Fedha.
Ametoa pongezi hizo wakati akipokea Jarida hilo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwamba alisema Jarida hilo ambalo limeendela kuwa bora na kufika kila mahali duniani kwa njia ya kidigitali ni nyenzo muhimu katika kuwasilisha taarifa sahihi, za wazi na kwa lugha inayoeleweka kuhusu shughuli, mafanikio na mipango ya Wizara ya Fedha.
Dkt. Mwamba alipongeza jitihada za Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na uelimishaji kwa umma pamoja na ubunifu na weledi unaooneshwa katika uandaaji wa Jarida hilo, akibainisha kuwa limeendelea kuwa chombo muhimu cha kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya fedha na uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake, Bw. Benny Mwaipaja alisema kuwa Jarida la Hazina Yetu linalenga kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha pamoja na mchango wake katika maendeleo ya Taifa, akiahidi kuendelea kuliboresha ili liwe chombo chenye tija zaidi katika mawasiliano ya serikali.
Jarida la “Hazina Yetu Toleo la Tano” limesheheni maarifa mbalimbali kupitia Makala bora kabisa, habari, matukio ya picha na matangazo mbalimbali na linapatikana kwa njia ya nakala ngumu (hard copies) na nakala tete (soft copies) kupitia mitandao ya kijamii ya Wizara na wadau wengine wa habari pamoja na Tovuti ya Wizara ya Fedha www.mof.go.tz

Post A Comment: