Ni katika Muendelezo wa  Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Monduli Ndugu Kisioki Lengoje Moitiko Katika kata ya Moita ambayo Jumla ya vikundi vilivyopo katika kata hiyo ni 47.

Akizungumza na Wanachama wa CCM na jumuiya zake ,ndugu Kisioki amesema lengo la ziara ni kushukuru baada ya kuchaguliwa na ni muendelezo wa ziara yake ambapo lengo kubwa ni kuwafikia wanachama wote , lakini pia kuwazesha Vikundi vya wanawake (vikundi,Vkoba) kiuchumi.

"Niwashukuru sana wanamoita kwani kati ya kata nilizotembelea yenye wanachama hai Moita ni Miongoni, lakini pia kina mama nawashukuru sana vikundi viko vingi sijui nitawagusaje kila mmoja lakini naomba nilichukue deni hili NAMI nikatafute Cha kuwafanyia wamama wa Moita , lakini wakati nachukua Deni Hilo Naomba niseme naomba viongozi wote wa Vikundi hivyo 47  ,Viongozi wa kata mnisaidie kuratibu hili Wamama hao wakaungane na wamama wingine Kisongo wapate mafunzo ya ujasiriamali na tutazungumza hukohuko ili kujua kila kikundi inajishulisha Na Nini ili tuone namna ya kuwasaidia na viongozi hao watakuja kuwapa mrejesho na kilichozungmzwa na kufundishwa, gharama zote usafiri ,Chakula Tutagharamia sipendi kufanya Kazi mwenyewe tushirikiane.". amesema Kisioki

Bitrice John Mandia ni katibu wa jumuiya hiyo Wilayani Humo , amesema ili uwe mwanachama hai lazima uwe na KADI ya Chama na Jumuiya zake , na kukusisitiza Umuhimu wa Elimu kwa Watoto wa Kike , na kuwasihi kina mama Kutoa taarifa sehemu husika pindi watakapogundua Mtoto wa kike kuozeshwa .

Prosper Damuni Meyani ni Diwani wa kata ya Moita ,yeye amesema Katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM, Serikali ya kata imesimamia kwa asilimia zote ikiwemo , ujenzi wa nyumba za Walimu Moita Bwawani,Umeme.

Nao baadhi ya wanachama na wananchi wa kata hiyo akiwemo Mwenyekiti wa UWT kata ya Moita wamemshukuru Kiongozi huyo wa Jumuiya ya wazazi kwa kutoa mwanga kuelekea mafunzo ya Ujasiriamali inayotarajiwa kuanza siku ya jumatano kuwa itakuaa chachu ya Maendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia miradi mbalimbali.



Share To:

Post A Comment: