Umoja wa Wanawake wa vyombo vya Ulinzi na Usalama Jiji la Dodoma kwa ushiriano na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ( General Hospital) wamefanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa kansa ya matiti na shingo ya uzazi. 


Vipimo hivyo vimefanyika jana Machi 24 Jijini Dodoma katika hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa (General hospital) kwa Lengo la kuhakikisha utunzaji wa afya njema kwa askari wote wanawake na kutatua changamoto za kiafya mapema. 


Aidha, Vipimo vingine vilivyofanyika kwa baadhi ya askari ni kipimo cha figo, kipimo cha ini na HIV/AIDS ambapo Askari 60 toka Polisi, Magereza na Zimamoto wakiongozwa na Naibu Kamishina wa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto Maria Kullaya, Kamishina Msaidizi wa Polisi Eva Stesheni ambaye ndiye mratibu wa zoezi hili akisaidiwa na Kamishina Msaidizi wa Magereza ELizabeth Mbezi.


Shukrani kwa Uongozi wa Hospital kwa kuratibu huduma za vipimo kwa askari na watumishi raia walio kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama. 


Zoezi hili ni endelevu litaendelea kutolewa kwa askari siku ya ijumaa tarehe 31,Machi, 2023 huku Mavazi ya kiraia yakivaliwa kwa ajili ya kutunza faragha za kitabibu.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: