Na;Elizabeth Paulo, Dodoma

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Linajivuni Mafanikio mbalimbali katika Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluh Hassan iliyotunga Sera mpya ya Mazingira ya mwaka 2021 ambapo kwa takribani miaka 24 hakukuwa na Sera mpya.


Baraza linatoshukrani kwa Serikali kwa kufanikisha kutunga Sera hiyo kutoka ile ya awali iliyopo ya mwaka 1997 iliokua haiendani na wakati na Mazingira ya sasa.


Mkurugenzi Mkuu (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa Majukumu ya Baraza pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita.


“Katika kipindi cha miaka 24 kumekua na changamoto nyingi ambazo ni mpya ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, Ongezeko kubwa la matumizi ya kemikali viwandani, tafiti za mafuta na gesi na biashara nzima ya mafuta na gesi kwahiyo Sera ya sasa hivi imetoa muongozo jinsi gani ya kukabiliana na hizi changamoto mpya ambazo hapo awali zilikua na hazipo.”Alisema Dkt.Gwamaka


Baraza limepata ithibati ya kuwa msimamizi wa kitaifa wa mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo Baraza na Halmashauri pamoja na Manisapaa mbalimbali zimekua zikishirikiana kuandika maandiko yanayopelekea kupata fedha za kutengeneza miundombinu katika Halmashauri husika kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Kadhalika Dkt. Gwamaka amesema Baraza limeendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuchangia zaidi ya shilingi bilioni 9 katika mfuko mkuu wa Serikali.



Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache Duniani zilizoweza Kudhibiti Matumizi ya mifuko ya plastiki ambapo Mheshimiwa Rais Samia alipokua Makamu wa Rais aliwezesha mchakato wa kuzuia Matumizi ya mifuko ya plastiki.


Aidha amesema Baraza imefanikiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa na ushirikiano mdogo miongoni mwa wananchi katika kusimamia sheria na Baraza kuendelea kutoa elimu ili wananchi waweze kuelewa na kusimamia suala zima la kuhifadhi na kutunza Mazingira kwaajili ya maendeleo endelevu.


Baraza imetoa namba za kupiga bila malipo kwa mtu yeyote Mwenye changamoto au maswali ya uchafuzi wa Mazingira 0800110116 pamoja na Baraza kuwa na jumla ya ofisi za Kanda 13 nchi nzima huku makao mkuu yakiwa Jijini Dodoma .


NEMC imetoa shukrani kwa Makamu wa Rais Dkt. Mpango, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Muungano na Mazingira Mh. Jaffo kwa kuendeleza kampeni za upandaji miti.


NEMC inaendelea kusimamia miradi ya kimkakati katika kufanya tathmini na athari za Mazingira kwenye maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: