Na. Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) leo Machi 03, 2023 limetoa Msaada kwa watu wenye mahitaji maalum, Wazee na Watoto yatima. Missionaries of Charity (Masista wa Upendo au Huruma) cha Mama Mtakatifu Teresia kilichopo Hombolo Jijini Dodoma ikiwa ni kuelekea kuazimisha siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2023


Akizungumza kwa niaba ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Makamu Mwenyekiti Naibu Kamishna wa Polisi DCP Maria Nzuki amesema wameona ni vyema kutoa msaada huo kwani ni utamaduni kwa Jeshi la Polisi kutoa misaada kwa vituo vya kulelea watoto yatima na makundi yenye uhitaji na kutoa mwaaliko kwa wananchi kuwa na destuli ya kutembelea na kutoa misaada katika vituo hivyo.




Mkuu wa kituo cha Mama Mtakatifu Teresia,ST. Prudencia Mc ambaye ni Sista mkuu amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwatembelea na msaada wao na kusema kuwa imekuwa faraja na furaha kwao na kusema kuwa kupitia msaada huo itawasaidia katika kuwatimizia mahitaji ya wahitaji maalumu hasa kwa watoto yatima na kulikaribisha tena Jeshi la Polisi kuwatembelea mara kwa mara kituo hapo.



Hata hivyo mmoja wa wahitaji wanaolelewa katika kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina la Tanasia Nonya amesema kwa niaba ya wenzake wanashukuru sana na kujisikia furaha kwa kutembelewa na kupewa msaada na Jeshi la Polisi na kuomba kutembelewa mara kwa mara na kuwakaribisha watu wengine kuwatembelea kituoni hapo.










PICHA NA BENEDICT MLAWA WA JESHI LA POLISI 

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: