Na,Jusline Marco:Arusha

Mahakama kuu kanda ya Arusha imeamuru walalamikiwa wa kesi ya jinai ya kupotea kwa Mzee Oriais Oleng'iyo (85) kufika mahakamani hapo pamoja na upande wa mletaji wa maombi hayo ambaye ni mtoto wa mzee Oriais, Machi 30 mwaka huu ili kesi hiyo iweze kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Mohamed Gwae iliyopangwa kuanza kusikilizwa Machi 22 mwaka huu imeahirishwa kutokana na upande wa walalamikiwa hao kutofika mahakamani hapo.

Walalamikiwa hao ambao wameshtakiwa kwa vyeo vyao ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Mkuu wa kituo cha polisi Wilaya ya  Ngorongoro,Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha, Mkuu wa jeshi la polisi nchini na Mwanasheria mkuu wa Serikali.

Naye mmoja wa Wakili upande Mlalamikaji Joseph Oleshangaiy akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo amesema Mzee Oriais alikamatwa na jeshi la polisi Juni 10 mwaka jana wakati wazoezi la uwekaji vigingi (Bikoni) katika eneo la vijiji 14 Loliondo Wilayani Ngorongoro na hadi sasa hajafikishwa mahakamani.

"Tunaamini kwamba mzee Oriais alikamatwa na polisi na hakuletwa mahamani kama ambavyo sheria inataka,inasadikika alikamatwa mwezi wa 6 mwaka jana wakati wa ile oparesheni ya Loliondo ya uwekeaji wa bikoni na mpaka sasa hajaletwa mahakamani."alisema Wakili huyo

"Na sisi tuyatimiza wajibu ambao mahakama imetupa wa kumleta mtoto wa mzee Oriais ili mahakama ipate uwezo wa kuona uhalisia tofauti na sisi mawakili lakini kwa familia hasa wale ambao kimsingi ndiyo wanaolalamika

Ameongeza kuwa ni muda mrefu umepita ambao sheria ilikuwa inataka afikishwe mahakamani ama kuachiwa huru kwani kwa umri wake wa zaidi ya miaka 85 na mufa aliokaa bila kujulikana alipo ni sababu tosha kwamba suala hilo lina maslahi kwa uma kwasababu ni binadamu na anahaki ya kuishi na familia yake kujua mahali alipo.

"Tulileta maombi haya kuomba mahakama itoe amri kuwalazimisha waliomshikilia au waliomuweka popote walikomuweka wamlete mahakami kama sheria inavyotaka kwani sheria zetu za jinai zinataka yeyote anayekamatwa kwa muda fulani lazima apelekwe kwenye vyombo vya sheria,kwahiuo kuna mbili aachiwe ama aletwe mhakamani."aliongeza wakili huyo

Hata hivyo kesi hiyo ya jinai imetokana na rufaa iliyoletwa awali mahakamani hapo ya kutaka watu zaidi ya 19 waliokamatwa Loliondo na mzee Oriais Oleng'iyo akiwa miongoni mwao mnamo Juni 10 mwaka jana wakati wa zoezi la uwekaji bikoni ambao waliachiliwa huru na kesi yao kufutwa huku mzee Oriais kutoonekana na kutojulikana alipo.

Simon Mbwambo,Willium Ernest na Joseph Oleshangaiy ambao ni mawakaili upande wa mlalamikaji wamesema moja kati ya maombi yao, wameiomba mahakama kuu kanda ya Arusha kuwaamuru walalamikiwa hao kuleta mwili wa Oriais akiwa hai au pasipo kuwa na uhai.

Mtetezi wa haki za binadamu Odero Odero ameeleza kuwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hii, moja ya haki ya msingi ni haki ya kuishi ambapo ameomba haki za binadamu ziendelee kuheshimiwa nchini na vyombo vyote vinavyohusika katika ulinzi wa haki za binadamu vitekeleze jukumu hilo.

"Hii ni kesi muhimu sana kwasababu nchi hii inaundwa na mtu mmoja mmoja haiundwi na watu hivyo ni lazima watu waweze kujua hilo,thamani ya maisha ya mtu moja katika taifa hili ni muhimu sana."Alisema mtetezi huyo wa haki za binadamu Odero Odero

Share To:

Post A Comment: